Friday, October 26, 2012

MAKABIDHIANO YA MADAWATI KATI YA UONGOZI WA NMB NA MBUNGE WA JIMBO LA MVOMERO, AMOS MAKALLA.

PICHA NA HABARI NA JOHN NDITI
UONGOZI NA KAMATI YA SHULE YA MSINGI, MASANZE ILIYOPO KATIKA KIJIJI CHA SANGA SANGA , KATA YA MZUMBE, WILAYA MVOMEO, UMEPATIWA MDAASA WA MADAWATI 50 KATI YA 76 KUTOKA NMB MAKAO MAKUU KUTOKANA JUHUDI ZA MBUNGE WA JIMBO LA MVOMERO, AMOS MAKALLA, AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO,

HII NI BAADA YA  KUUOMBA UONGOZI HUYO KUSAIDIA MADAWATI KATIKA SHULE KADHAA ZA MSINGI JIMBONI MWAKE. MSAADA HUO UMETOLEWA BAADA YA ZIARA YA MBUNGE HIYO KUANDIKA BARUA YA KUIOMBA BENKI HIYO WAKATI ALIPOJIONEA MWENYEWE HALI MBAYA YA UHABA WA MADAWATI WAKATI WA ZIARA KATIKA VIJIJI KADHAA IKIKIWEMO CHA SANGA SANGA.

NA OKTOBA 25,MWAKA HUU NMB ILITIMIZA UTEKELEZAJI WA MAOMBI HAYO KWA MKUMKABIDHI MBUNGE HUYO MADAWATI 76. KATI YA MADAWATI HAO , 50 WALIPEWA UONGOZI WA SHULE HIYO ILI KUPUNGUZA TATIZO SUGU LA UHABA WA MADAWATI NA YALIYOSALIA YAMEPANGIWA KUISAIDIA SHULE NYINGINE AMBAYO NAYO IMEKUBWA NA UHABA MKUBWA WA MADAWATI.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, ( kati kati ) akiwa ameketi kwenye dawati, na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki hiyo, Gabriel Ole Loibanguti  (kushoto) na ( kulia) ni  Mwalimu Mkuu wa Shule ,Leochrista Bavon, ni baada ya makabidhiano ya madawati 50 kati ya 76 yaliyotolewa na NMB kufuatia maombi ya msaada wa Mbunge huyo ili kukabiliana na uhaba wa madawati kwenye baadhi ya shule za Msingi Jimboni humo, hafla iliyofanyika shuleni hapo, Oktoba 25, mwaka huu.
Kukata utepe
 Wanafunzi
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo,  ( kushoto) akipeana mkono na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya NMB , Gabriel Ole Loibanguti , Oktoba  25, mwaka huu  ikiwa ni ishara ya  makabidhiano ya  msaada wa madawati 50 kwa shule ya Msingi Masanze,iliyopo  Kijiji cha Sanga Sanga, Kata ya Mzumbe, kufuatia ombi la Mbunge huyo kwa Uongozi wa makao makuu ya Benki hiyo hivi karibuni  (kati kati ) ni Mwalimu Mkuu wa Shule  hiyo ,Leochrista Bavon.
 Furaha
 Wanafunzi na mfadhili wao
 Mwalimu akishukuru kwa msaada
 Picha ya pamoja na walimu


No comments: