Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda
kuwataarifu kuwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura ameteuliwa na Shirikisho
la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa watakaoshughulikia
masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake
zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou
kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo za Mataifa ya Afrika
kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika Novemba
11, 2012.
Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia
habari kwenye fainali hizo. Wengine ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF,
Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.
Wambura atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye Kamati ya
Maandalizi ya fainali hizo, kitu ambacho TFF inajivunia kutoa mwakilishi
kwenye moja ya mashindanoi makubwa ya mpira wa miguu Tanzania.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga ameelezea uteuzi
huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri ambayo Wambura amekuwa akiifanya
tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka 2011.
“Taarifa zake mbalimbali zimeifanya Tanzania iwe
inang’ara CAF na hata FIFA kwa kuwa kwa sasa wanajua kila kinachoendelea
kwenye soka la Tanzania,” alisema Rais Tenga na kumtakia Wambura kila
la kheri kwenye kazi hiyo atakayoifanya kwa takriban siku 14.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, akizungumza kwa
niaba ya Sekretarieti, amemtakia Wambura kazi njema na kwamba awe kioo
cha mabadiliko makubwa yanayoendelea kwenye soka la Tanzania.
Wambura alijiunga na TFF Januari, 2011 akiwa mmoja
wa waajiriwa watatu wapya kwenye Shirikisho baada ya wsatendajiu wengine
wawili kumaliza muda wao wa mikataba.
Wambura ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye ameshafanya
kazi kwenye vyombo mbalimbali kuanzia kazi ya uandishi hadi Mhariri
Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo ambalo alikuwa akifanya kazi kabla ya
kujiunga na TFF
Mahmoud
Garga (CAF)
Boniface
Wambura (Tanzania)
Arlindo Macedo (Angola
No comments:
Post a Comment