Sunday, September 9, 2012

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA

 01.                        Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kabla ya kuanza ziara yake ya siku 3 kutembelea Viwanda Mkoani humo.
 01.                        Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akionesha kukubaliana na Maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha kuzalisha mifuko na maturubai cha Pee Pee kilichopo Mkoani Tanga
 01.                        Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda( Katikati), Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Bi Halima Dendegu na watendaji wengine wa Mkoa Tanga wakipokea taarifa ya hali ya mgodi wa malighafi za kuzalisha saruji ya Lime stone unaomilikiwa na kiwanda cha Saruji Tanga.
              Mgodi wa malighafi za kuzalisha saruji( limestone) ambao umekuwa ukitoa malighafi hizo tangu kuanzishwa kwa Kiwanda hicho miaka zaidi ya 30 iliyopita. Tafiti zinaonesha kuwa, malighafi hiyo itaendelea kupatikana kwa zaidi ya miaka 130 ijayo.
 01.                        Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Ukanda wa Uwekezaji wa Kiuchumi wa Mkoa wa Tanga Bw Chris Chae. Uwekezaji mkubwa unatarajiwa kuanza katika eneo hilo hivi karibuni.
             Mashine za kisasa za kusaga na kupanga unga katika Viwango mbali mbali zilizopo katika Kiwanda cha Unga cha Pembe kilichopo Mkoani Tanga.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Dkt Abdallah Kigoda, yupo katika ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea Viwanda  Mkoani Tanga.
Ziara hiyo ni maalum kwa lengo la kuvitembelea Viwanda ili kujionea utendaji wake na kuhimiza utendaji zaidi kwa sekta hiyo yenye mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi, ajira na pato la Taifa.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Dkt Kigoda ametembelea Viwanda vya Saruji Tanga na  Athi River, Kiwanda cha mifuko na maturubai cha Pee Pee, Kiwanda cha Unga wa ngano cha Pembe na Ukanda huru wa Uwekezaji Kiuchumi wa Mkoa wa Tanga.
Katika maeneo yote hayo, Waziri Kigoda amesifu juhudi za Uongozi wa Mkoa wa Tanga katika kufufua Viwanda vya zamani, kuibua fursa zilizopo katika sekta hiyo kwa kuanzisha Viwanda vipya pamoja na kampeni kubwa ya kuhimiza  uwekezaji inayofanywa na Mkoa huo.
Ameahidi jitihada zaidi zinafanywa na serikali katika kuongeza ufanisi wa sekta za Nishati hasa upatikanaji wa gesi na Umeme, miundo mbinu ya barabara, reli na bandari na ushiriki wa asasi za fedha katika kutoa mitaji ili kuisaidia sekta ya Viwanda kutoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi.
Ziara hiyo ya Waziri Kigoda na wasaidizi wake kutoka Wizarani imeendelea Jumapili hii kwa kutembelea Viwanda mbali mbali.

No comments: