Friday, September 21, 2012

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA NA NAIBU WAKE WATEMBELEA MAJENGO MAPYA YA TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO (LAW SCHOOL OF TANZANIA) LEO

Mhe. Mathias Chikawe (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Naibu wake Mhe. Anjellah Kairuki (Mb) leo tarehe 21/9/2012 wametembelea majengo mapya ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) yaliyoko katika kiwanja Na 2005/2/1, Sinza, Barabara ya Sam Nujoma/Barabara ya Mpakani. Nia ya ziara hiyo ilikuwa kuona maendeleo ya ujenzi wa Taasisi ambayo awamu ya kwanza ya ujenzi wake ilianza Tarehe 18 Novemba 2010. Ujenzi huo unafadhiliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Program ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (Legal Sector Reform Program) na mpaka sasa umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 16.1. Ujenzi huo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 98 na umehusisha ujenzi wa jengo la Utawala, Jengo la Madarasa, Jengo la Maktaba, jengo la Mahakama ya Kujifunzia, Kantini, Ukumbi wa Shughuli mbalimbali na Nyumba za kuishi. Mkuu wa Taasisi Hiyo Mheshimiwa Judge Dkt. Gerald Ndika aliwaeleza Mawaziri kuwa Taasisi hiyo ilihamishia shughuli zake za ufundishaji na utawala katika majengo hayo Agosti Mwaka huu baada ya sehemu kubwa ya ujenzi na ununuzi wa samani kukamilika. Kufuatia kukamilika kwa majengo hayo kwa sasa Taasisi itakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi mpaka elfu mbili kwa mwaka tofauti na wanafunzi mia tano mpaka mia sita ambao walikuwa wakidahiliwa siku za nyuma.
Mhe. Mathias Chikawe (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria akitembelea  majengo mapya ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) yaliyoko katika kiwanja Na 2005/2/1, Sinza, Barabara ya Sam Nujoma/Barabara ya Mpakani
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Anjellah Kairuki (Mb) leo tarehe 21/9/2012 akipanda mti walipotembelea majengo mapya ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) yaliyoko katika kiwanja Na 2005/2/1, Sinza, Barabara ya Sam Nujoma/Barabara ya Mpakani. 
Majengo mapya ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) yaliyoko katika kiwanja Na 2005/2/1, Sinza, Barabara ya Sam Nujoma/Barabara ya Mpakani.
Mhe. Mathias Chikawe (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Naibu wake Mhe. Anjellah Kairuki na uongozi wa Taasisi hiyo katika ukumbi wa masomo


Mhe. Mathias Chikawe (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Naibu wake Mhe. Anjellah Kairuki wakitembezwa kwenye majengo ya taasisi hiyo

Majengo mapya ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) yaliyoko katika kiwanja Na 2005/2/1, Sinza, Barabara ya Sam Nujoma/Barabara ya Mpakani.

Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mhe. Chikawe ambaye aliwasihi wanafunzi kulinda miundo mbinu ya taasisi hiyo na kuitumia kwa ukamilifu ili waweze kufaulu na kuongeza wigo wa wananchi kupata huduma za kisheria nchini.


Mhe. Mathias Chikawe (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria akipanda mti 

No comments: