|
Mwalimu wa Ujasiriamali kutoka katika Taasisi ya RafikiElimu Foundation, Mama Ashankira Lupembe , akifundisha kwa vitendo namna ya kutengeneza sabuni ya maji. | |
|
Mwanafunzi wa ujasiriamali akitengeneza sabuni ya unga mwenyewe mara baada ya kupata maelekezo kutoka kwa waalimu wa ujasiriamali kutoka RafikiELIMU Foundation. | |
|
Mwanafunzi wa ujasiriamali akitengeneza sabuni ya maji kwa vitendo mara baada ya kupata maelekezo kutoka kwa waalimu wa Ujasiriamali kutoka katika Asasi ya RafikiElimu Foundation. | |
|
Wajasiriamali wakifanya " practical " ya kutengeneza sabuni ya maji kwa vitendo mara baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa waalimu wa ujasiriamali kutoka katika Asasi ya RafikiElimu Foundation. |
|
|
Mwalimu wa Ujasiriamali kutoka Taasisi ya RafikiElimu Foundation, Mama Hellen Mbise akielekeza kwa vitendo namna ya kutengeneza sabuni za maji. |
|
|
Mwalimu Ashankira Lupembe akiwaonyesha wanamfunzo kitambaa kilcho fuliwa kwa kutumia sabuni aliyo itengeneza mwenyewe wakati wa uzinduzi wa EUMIVI PROJECT. |
|
|
Mwalimu wa Ujasiriamali kutoka Taasisi ya RafikiElimu Foundation, Mama Ashankira Lupembe akifua kitambaa kwa kutumia sabuni iliyo tengenezwa wakati wa mafunzo ya utengenezaji sabuni ya wakati katika uzinduzi wa mradi wa Elimu ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini. | |
|
Mama Ashankira Lupembe, Mtaalamu na Mwalimu wa Ujasiriamali kutoka RafikiElimu Foundation akitoa maelekezo ya namna ya kutengeneza sabuni ya maji kwa vitendo. |
|
Mradi uliolenga kupunguza tatizo la ajira nchini kwa kutroa elimu ya ujasiriamali kwa maelfu vijana wa kitanzania waishio mijini na vijijini ifikapo mwezi Novemba 2014 umezinduliwa rasmi leo jijini Dar Es salaam. Uzinduzi huo ulio fanyika mapema leo katika eneo la Shule Ya Msingi Mlimani iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam na kuhudhuriwa na makumi ya vijana wa kada mbalimbali jijini Dar es salaam uliambatana na mafunzo ya ujasiriamali ambapo wahudhuriaji walipata nafasi ya kujifunza kutengeneza sabuni za aina mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa kutoka katika taasisi ya RafikiElimu Foundation, taasisi inayo jihusisha na maendeleo ya jamii.
|
Baadhi ya wajasiriamali walio hudhuria katika Uzinduzi wa Mradi wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini uliofanyika leo jijini Dar Es salaam. |
|
Akiulezea mradi huu, mratibu msaidizi wa mradi huo alisema kuwa mradi huu upo katika awamu kuu mbili. Awamu ya kwanza itafanyika kuanzia tarehe 01 Septemba 2012 hadi tarehe 29 Septemba 2012, na utafanyika katika mikoa ya Dar Es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Dodoma na Kilimanjaro, ambapo mbali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali, asasi itatafuta vijana kumi na wawili kutoka katika hiyo mikoa saba kwa ajili ya kufanya kazi kama wajitoleaji " volunteers" katika awamu ya pili ya mradi itakayo anza rasmi tarehe 01 Novemba 2012 na kuchukua miaka miwili hadi Novemba 2014 ambapo ndipo itakapo kuwa tamati ya mradi huu.
Awamu ya kwanza ya mradi huu inafanyika katika mikoa ya Dar Es salaam, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Dodoma, Mwanza na Mbeya. Jijini Dar Es salaam, mafunzo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 01 Septemba 2012 hadi tarehe 04 Septemba 2012 katika Shule ya Msingi Mlimani , iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam... Ratiba kamili ya awamu ya kwanza ya mafunzo haya ni kama ifuatavyo :
1. ARUSHA, MOSHI & MOROGORO : Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Septemba 2012.. Mwisho wa kujiandikisha katika " programme hii " kwa wakaazi wa ARUSHA, MOSHI na MOROGORO ni tarehe 15 Septemba 2012.
|
Baadhi ya wanafunzi wa ujasiriamali waliohudhuria katika mafunzo haya wakifuatilia darasa kwa makini.
|
|
MWANZA, MBEYA & DODOMA : Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Septemba 2012.
Mwisho wa kujiandikisha katika programme hii kwa wakaazi wa DODOMA, MBEYA & MWANZA ni tarehe 25 Septemba 2012.
No comments:
Post a Comment