Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari jijini Dares Salaam wakiandamana kimyakimya kuelekea viwana vya Jangwani ikiwa ni hatua ya kuonyesha hisiazao za kupinga mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia.
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,Nevil Meena akitoa muongozo wa njia ya kupita wakati wa Maandamano hayo leo.
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,Nevil Meena akitoa Tamko.
Tamko lililotolewa na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nevil Meena, kuhusu maandamano hayo,
"Kunawatu wanahoji tunaandamana alafu iweje wakati siye ndio wenye vyombo vya habari si tuandike tu? Hapana kuandamana kwetu kunamaana sana tumeandamana sikama hatuna uwezo wakufanya kitu zaidi ya kuandamana, tunazo silaha kubwa zaidi ya maandamano lakini hii ni hatuayapili baada ya matamko mbalimbali kutolewa.
Aidha meena akahoji hivyo inakuaje kama sikumoja watu wakaamka wakakuta hakuna chombo chochote cha habari kilicho hewani hakuna tv, hakuna radio na wala hakuna magazeti nchi hii itakuwaje?
Wanahabari waendelee kuwa na utulivu hatua mbalimbali zitakazoendelea kuchukuliwa watafahamishwa kuhusiana na tukio hilo."
Vingozi wengi wa vyama vya waandishi wa habari waliotoa maoni yao kwenye mkusanyiko huo waliitaka serikali wachukue hatua na damu ya Mwangosi iwes shule kwao.
Mhariri Mtendaji wa Channel Ten,Dinah Chahali akizungumza.
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari jijini Dares Salaam wakiandamana kimyakimya kuelekea viwana vya Jangwani ikiwa ni hatua ya kuonyesha hisiazao za kupinga mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia.
Waandishi wakiigiza tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi namna lilivyotokea huko Iringa wakati wa maandamanoyao yalioanzia kwenye ofisi za Chanel ten hadi jangwani leo asubuhi.
Wazee wa Feva nao hawakua nyuma kufatilia Maandamano hayo.
Waziri wa Ulinzi Emmanuel Nchimbi akizondolewa kwenye mkusanyiko wa waandishi wa habari baada ya kukataliwa kuzungumza chochote kutokana na kutoalikwa kwenye mkutano huo. Waandishi wa habari walishangazwa na kuwepo kwake wakati hakukua na kiongozi yeyote aliyealikwa kutoka serikalini.
Mwandishi wa habari na mhariri Manyerere Jackton, akizungumza mbele ya waandishi wa habari wenzake na kutoa maoni na ushauri wa nini chakufanya.
No comments:
Post a Comment