Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa
Makampuni ya ASAS, Salim Abri kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho hayo
ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa. Abri pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Redio
One na Capita Radio, Deogratius Rweiyunga kwa mchango wake wa kufanikisha
Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani Kitaifa mkoani Iringa.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa
Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Geita, Willson Msuka kwa mchango wake wa
kufanikisha Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa
Baadhi
ya madereva wa Pikipiki mkoani Iringa waliopatiwa mafunzo maalum ya uendeshaji
pikipiki na kufaulu wakila kiapo cha utii wa sheria za barabarani mbele ya
Mgeni rasmi.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akifunga rasmi maadhimisho ya Wiki
ya Nenda kwa Usalama Kitaifa Mkoani Iringa leo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Iringa Ritha Motto Kabati (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
Wasanii wa kundi la Mizengwe wakitoa burudani katika sherehe za ufungaji wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa Mkoa wa Iringa. Kulia ni Mkaguzi wa Polisi, Abel Swai.
Afisa
Mwandamizi wa Mawasiliano kwa Umma wa SUMATRA, Maria Msellem, (kushoto)
akitoa maelezo juu ya namna ya matumizi sahihi ya kufuata sheria za
barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara kwa
Mgeni rasmi katika ufungaji wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa, Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa anatembelea banda
la Posili usalama barabarani leo katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Mwenyekiti
wa Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga
maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Iringa Ritha Motto Kabati (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Meneja
Mauzo wa Airtel, Kanda ya Nyanda za Kusini, Beda Kinunda mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo
kitaifa. Airtel ndio wadhamini wa maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na RPC wa Mkoa
wa Mbeya, Diwani Athuman mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora
mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akipokea zawadi ya Airtel
kutoka kwa Meneja Mauzo wa Airtel, Kanda ya Nyanda usini, Beda Kinunda
mara baada ya kutembelea banda la Airtel ambao ndio wadhamini wakuu wa
wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. Kulia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani,
Pereira Silima.
Wabunge
wa Viti Maalum mkoa Iringa, Ritha Motto Kabati (kulia) na Ckiku Alfan
Abwao (kushoto) wakiwa katika viwanja vya Samora mjini Iringa hii leo
katika ufungaji wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa.
Mwanafunzi
wa darasa la sita Shule ya Msingi Malangali Mkoani Iringa, Steven
Mligo(kushoto) akitoa maelezo juu ya namna ya matumizi sahihi ya kufuata
sheria za barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa
barabara kwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Wiki ya Nenda kwa Usalama
Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa
anatembelea banda la Polisi usalama barabarani leo katika uwanja wa
Samora mjini Iringa.
Ofisa
wa Wizara ya Ujenzi, (kulia akitoa maelezo ya Wizara hiyo kwa Mgeni
Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea
banda hilo. Kushoto kabisa ni Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Barabara TANROAD wakiwa katika banda lao
Mkurugenzi
wa Mipango wa TANROADS, Mhandisi, Jason Rwiza (kushoto) akitoa maelezo
ya taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine
Ishengoma alipotembelea banda hilo. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi
Gerson Lwenge
Meneja
wa Mkoa wa Iringa wa Shirika la Bima la Taifa, (NIC) Ally Mohamed
(kulia) akitoa maelezo ya taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Wengine ni
Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati (kushoto) na Kamanda wa
Trafiki, Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga.
Afisa
Mauzo Msaidizi wa ASAS, Stanley Nyamle (kushoto) akitoa maelezo juu ya
namna ya matumizi sahihi ya kufuata sheria za barabara kwa watembea kwa
miguu na watumiaji wengine wa barabara kwa Mgeni rasmi katika ufungaji
wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk.
Christine Ishengoma alipokuwa anatembelea banda la Polisi usalama
barabarani leo katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Wanafunzi wakitumbuiza kwa nyimbo katika kilele hicho cha Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mjini Iringa hii leo.
Wabunge
wa Viti Maalum mkoa Iringa, Ritha Motto Kabati (kulia) na Ckiku Alfan
Abwao (kushoto) wakifurahia jambo katika viwanja vya Samora mjini Iringa
hii leo katika ufungaji wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama
Kitaifa.
Wasanii wa kundi la Mizengwe wakitoa burudani katika sherehe za ufungaji wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa Mkoa wa Iringa. Kulia ni Mkaguzi wa Polisi, Abel Swai.
No comments:
Post a Comment