Wednesday, September 26, 2012

Jumuiya za Uingereza- Tanzania zasherekea miaka 50 ya utaifa

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mh Balozi Dr Diodorus Kamala akifanunua kuhusu maendeleo katika nchi ya Tanzania wakati wa hafla hiyo ya kusherehekea miaka 50 utaifa kati ya Tanzania na Uingereza.

Salam, 

Siku ya jumanne tarehe 25.9.12 Jumuiya ya Uingereza- Tanzania ( BRITAIN- TANZANIA SOCIETY) iliandaa hafla fupi ya kusherekea miaka 50 ya Utaifa kati ya Nchi ya Uingereza na Tanzania katika ukumbi wa The Royal Commonwealth Club, London. 

Wageni mbalimbali pamoja na wanachama walijitokeza kwa wingi kuhudhuria hafla hii fupi ilioandaliwa hususani kwa ajili ya kuchangia nchi ya Tanzania. Mojawapo ya wageni waliohudhuria ni pamoja na balozi wetu Peter Kallaghe pamoja na mkewe Mama balozi Joyce Kallaghe, Mwenyekiti wa Britain- Tanzania Society William Fulton JP DL. 

Mgeni rasmi katika shughuli hii alikua ni Balozi wa Ubelgiji Mh Dr Diodorus Kamala aliyetoa mada maalum kuhusu mafanikio, maendeleo na changamoto katika nchi ya Tanzania na jumuiya nzima ya Afrika mashariki. Aidha Mh Dr Kamala alifafanua jinsi uchumi wa Tanzania unavyokua kwa kasi kutokana na takwimu kutoka Benki ya Dunia pia aliongelea kuhusu masuala ya utalii, mioundo mbinu, hali ya amani na usalama ambazo zimepelekea wawekezaji wengi kuwekeza katika nchi ya Tanzania. 

Nchi ya Uingereza ndio nchi pekee inayoongoza katika uwekezaji katika nchi ya Tanzania Ikifuatiwa na India pamoja na Kenya Pamoja na hayo Mh Dr Kamala aliwashukuru wana jumuiya wa Uingereza- Tanzania kwa kuendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali ili kupambana na hali ya umaskini. 

Baada ya kutoa mada yake kulikuwa na kipindi kifupi cha maswali na majibu kutoka kwa wanajumuiya pamoja na wadau waliohudhuria. Nae mwenyekiti wa Computer 4 Afrika ndg Aseri katanga alitoa risala fupi ya kumshukuru mgeni rasmi kwa kujitolea kwake kuja kujumuika na wanajumuiya pamoja na hotuba yake nzuri kuhusu Tanzania. 

Vile vile halfa hii ilijumuisha uoneshwaji wa picha zilizochorwa na wachoraji kutoka Tanzania ambazo zilinadiwa ili kuchangisha pesa za kuwasaidia kuwainua wadau wa tasnia ya uchoraji Tanzania. Baadhi ya wachoraji ambazo picha zao zilionyeshwa ni Mmadi Ausiy, Haji Chilonga, Hassan Kadudu, Florian Ludovick Kaija, James Haule na Aggrey Mwasha. 

 Asanteni, 
Urban Pulse Creative
Mkutano Ukiendelea.
Msanii Francia Chengula akiimba wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa Computer 4 Afrika (katikati) Aseri Katanga akifuatilia mada ya Mh Balozi Kamala.
Mwenyekiti wa Computer 4 Afrika Aseri Katanga akisoma risala fupi ya kumshukuru Mgeni Rasmi na wageni waalikwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uingereza- Tanzania William Fulton JP DL akiongea na Urban Pulse baada ya Mkutano.
wadau wakibadilishana mawazo pamoja.
Balozi Dr Kamala akiwa na Sir Andy Chande.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh Peter Kallaghe akiwa na Susan Mzee na Sheilamina
Mama Balozi Joyce Kallaghe katika picha ya Pamoja Nelly Sheilamina na Elly baada ya mkutano.
Mh Balozi Dr Diodorus Kamala (Kulia) Frank Eyembe na Aseri Katanga.

No comments: