Waziri
wa Katiba na Masuala ya Sheria, Mhe. Mathias Chikawe ( Mb ) akipitia
kwa mara ya mwisho hotuba yake kabla ya kuisoma, wakati wa mkutano wa
kilele wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukajadili Utawala wa Sheria katika
Ngazi ya Kimataifa na Kitaifa, katika hotuba yake katika mkutano huo
ambao ulifunguliwa na Katibu Mkuu, Ban Ki Moon, na kuhutubiwa na
Viongozi wakuu wa nchi na serikali wakiwamo Mawaziri kutoka nchi 80,
alielezea namna ambavyo Jamhuri ya Muungano imekuwa ikizingatia utawala
wa sherika katika ngazi ya taifa, kanda na kimataifa na akaelezea pia
mchakato unaoendelea wa maandalizi ya Katiba mpya. wengine katika picha
kuanzisha kulia ni Mhe. Abubakari khamisi Bakari,(Mb) Waziri wa
Sheria na Masuala ya Katiba kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mhe, Musa Hassan Mussa ( Mb) kutoka Zanzibar na waliokaa nyuma ni
wataalam wa sheria.
Mhe.
Mathias Chikawe ( Mb) akihutubia Mkutano wa Kilele wa Umoja wa
Mataifa uliokuwa ukijadili ajenda ya Utawala wa Sheria katika ngazi ya
Kitaifa na Kimataifa. Mkutano huo wa Siku Moja ulifanyika siku ya
Jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum
Waziri
wa Katiba na Masuala ya Sheria Mathias Chikawe ( Mb) amesema, Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania imejidhatiti ipasavyo katika utekelezaji na
uzingatiaji wa utawala wa sheria kuanzia ngazi ya taifa, kanda na
kimataifa.
Chikawe ameyasema hayo jana jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa, katika Mkutano wa kilele ambao ajenda yake kuu ilikuwa ni
Utawala wa Sheria kitaifa na Kimataifa”.
Mkutano
huo ambao umeandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki
Moon, umehudhuriwa na kuhutubiwa na viongozi wakuu wa nchi na serikali
na mawaziri zaidi ya 80 wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Hii
ni mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa kuandaa mkutano
wa aina hii ambao ulijikita katika kuzungumzia utawala wa sheria kama
kiungo muhimu kati ya ngazi ya kitaifa na kimataifa na ukuaji wa
uchumi, maendeleo endelevu na kuondoa umaskini na njaa
Aidha mkutano huo pia umetoa fursa kwa nchi kuelezea namna gani
zimekuwa zikizingatia au kutekeleza utawala huo katika ngazi ya
kimataifa na kimataifa.
Mkutano
huu umefanyika siku moja, kabla ya kuanza kwa majadiliano ya Mkutano
wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mkutano utakaofunguliwa leo
siku ya Jumanne, utahutubiwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais wa
Marekani Barack Obama.
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano huu wa 67 unaongozwa na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe(Mb) akimwakilisha
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri
Mathias Chikawe ni miongoni wa wajumbe wanaohudhuria mkutano huu
akiwamo pia Mhe. Abubakari Khamis Bakali (Mb), Waziri wa Katiba na
Masuala ya Sheria kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Vita
Kawawa ( Mb) na Mhe. Musa Hassan Musa ( Mb) kutoka Zanzibar
Akizungumzia utawala wa sheria katika ngazi ya kitaifa, Waziri Mathias
Chikawe amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, utawala wa sheria ni
sehemu ya makubaliano ya kijamii kati ya taifa na mtu binafsi.
“
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imekuwa nguzo
muhimu katika kutoa mwongozo na kipimo cha utawala bora. Na kwa
sababu hiyo misingi ya usawa mbele ya sheria, uwajibikaji kwa sheria
na mgawayo wa madaraka vimezingatiwa katika utawala wa sheria” akasema
na kuongeza
“ Kwa kuzingatia kwamba Katiba inatokana na wananchi na inazingatia
kile ambacho wananchi wanataka, Tanzania hivi sasa iko kazi zoezi
linalohusisha kila mtu kupitia Katiba ya sasa kwa alengo la kuanda
katiba mpya baada ya Katiba ya sasa kuitumikia Tanzania kwa miaka 50
iliyopita”.
Ameeleza.
Aidha
Waziri Chikawe amesema Katiba ya Tanzania pia imetoa nafasi ya
kuanzishwa kwa taasisi za kitaifa zenye wajibu wa kuhakikisha kwamba
utawala wa sheria siyo tu unafuatwa lakini pia haki za wananchi
zinalindwa
Akabainisha kwamba baadhi ya taasisi za aina hiyo ni Kamisheni ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, taasisi ambayo kwa miaka mingi imeendelea
kufanya kazi nzuri.
Akaongeza
kwamba uzingatiaji wa misingi ya ulinzi na uhifadhi wa haki za
binadamu, fursa ya kupata haki na uasawa, utawala bora na utawala wa
sheria nchini ni mambo ambayo yamezingatiwa vema katika Dira ya taifa
ya mwaka 2025 na Mpango wa Taifa wa Kukuza uchumi na Kupunguza
Umaskini.
Katika
hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Utawala wa Sheria amesema,
uimarishaji wa mfumo wa sheria ni moja yamambo ambayo yamepewa
kipaumbele katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
Na kwamba serikali imefanya jitihada za makusudi za kuongeza idadi ya
majaji, mahakimu, ujenzi wa mahakama mpya na kuzikarabati za zamani.
Akaeleza
pia kwamba kumekuwa na mikakati ya kuboresha huduma za mahakama
kwa kuanzisha huduma itakayojulikana kama tele justice.
Aidha akauelezea umma huo wa Umoja wa mataifa, kwamba Tanzania
imejipanga kupambana kikamilifu na rushwa ili kuwa na jamii huru.
Awali akufunguaa mkutano huo ambao mwishoni ulipitisha Andiko, Katibu
Mkuu Ban Ki Moon alitoa mwito kwa jumuia kushirikiana na kwa kutumia
sheria ya kimataifa, kutatua migogoro kwa njia ya zamani na kuhakikisha
kwamba mgogoro hiyo haitokei tena.
Aidha
Katibu Mkuu amezitaka nchi kuimarisha utawala wa sheria ikiwa ni
pamoja na kuwapatia mafunzo ya polisi na kuimarisha idara ya mahakama
hususani katika nchi zile ambao hali ya amani ni tete na zimekuwa
zikikumbwa na migogoro.
Kwa upande wake, Rais wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa Bw. Vuk
Jeremic ameonya dhidi ya kuona sheria ya kimataifa kama nyenye umuhimu
mdogo na inamadhara kwa uendeshaji wa masuala ya dunia
Akasisitiza kwamba kama nchi na watawala watakuwa madhubuti na
kuzingatia utawala wa sheria ni wazi hakuta kuwapo na ushawishi wa
kukimbilia vita.
Akasisitiza
umuhimu wa uwepo wa Makama ya Makosa ya Jinai (ICC) na kuzitaka
nchi ambazoa hazijaitambua mahaka hiyo au kuiona kama si sehemu ya
Umoja wa Mataifa kuachana na dhana hiyo
Akasema kazi ya ICC ni pamoja na kuhakikisha kwamba haki inatendekea
kwa kuwafikisha mbele ya mahakama hiyo watuhumiwa wa makosa ya jinai
na kuzuia kutoa jirudia kwa mauaji ya kimbari.
Aidha
mkutano huo pia ulihutubiwa na viongozi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa kama vile Kamisheni ya Haki za Binadamu, Rais wa Mahakama ya
Kimataifa ) ICJ Bw Petro Tomka ambaye alibainisha kwamba ni nchi 67 tu
kati ya Nchi 193 za Umoja wa Mataifa, sawa na asilimia 34 ikiwa ni
pamoja na mwanachama mmoja tu wa Baraza kuu la Usalama ambazo
zimeikubali na kuitambua ICJ.
No comments:
Post a Comment