Wednesday, July 18, 2012

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KATIKA SEHEMU ZA HISTORIA ZANZIBAR

Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali akiwaelezea Wanahabari hawapo pichani mambo mbalimbali ya Historia ya Zanzibar ndani ya Nyumba ya Baitil Ajabu hapo Forodhani ikiwa ni Mwanzo wa Ziara ya Waandishi kutembelea Sehemu mbalimbali za Historia ya Zanzibar.
Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali akiwanesha waandishi Ramani ya Mji wa Zanzibar ulivyokuwa kabla na kubainisha mabadiliko mbalimbali yaliotokea.
Waandishi wakiangalia Picha ya Kasri ya Mwinyi Mkuu Pamoja na Bakuli yake ya kunywea Uji ambayo ipo hadi sasa ndani ya Nyumba ya Baitil Ajab Forodhani mjini Zanzibar.
Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali walifika huko maruhubi na kupata historia ya majengo hayo ambaya yalijengwa na Mfalme Baraghash kwa ajili ya Starehe tu katika mwaka 1880 na kuharibika kwa kuungua moto mwaka 1889.
Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali walifika huko maruhubi na kupata historia ya majengo hayo ambaya yalijengwa na Mfalme Baraghash kwa ajili ya Starehe tu katika mwaka 1880 na kuharibika kwa kuungua moto mwaka 1889.
Hichi ndio kisima cha Chini kwa chini kilichokuwepo huko Mangapwani Mkoa wa kaskazini Unguja.
Waandishi wa Habari wakiwa Ndani ya Kisima cha Chini kwa chini chenye Urefu wa zaidi ya Kilomita moja katika kila pembe ya ndani ya kisima hicho.
Wanahabari wakiingia ndani ya Handaki lililojengwa na Utawala wa Kikoloni kwa ajili ya kujilinda na Vita Mwaka 1939-1945.
Hili ndilo handaki lililojengwa na Utawala wa Kikoloni kama linavyoonekana kwa ndani.
Hii ni nyumba ya chini kwa chini iliojengwa na Waarabu kwa ajili ya maficho ya Watumwa baada ya kupigwa marufuku Biashara hio mwaka 1873 huko katika kijiji cha Mangapwani kaskazini Unguja.
Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali akiwaongoza Waandishi kuingia ndani ya Nyumba ya chini kwa chini iliojengwa na Waarabu kwa ajili ya maficho ya Watumwa baada ya kupigwa marufuku Biashara hio mwaka 1873 huko katika kijiji cha Mangapwani kaskazini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments: