Monday, July 2, 2012

WASHIRIKI WA TANZANIA WATIA FORA MAONESHO YA 48 YA BIASHARA YA KIMATAIFA NDOALA NCHINI ZAMBIA

 Wajasiriamali Kumi na Moja wa Kikundi cha HANDCRAFTS OF TANZANIA HOT) wakiwa mjini Ndola nchini Zambia, walishiriki Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa. Maonesho haya yalianza tarehe 27 Juni 2012 na yanategemea kumalizika tarehe 03 Julai 2012 Pichani ni  wajasiriamali wetu katika picha ya pamoja na Mhe. Grace J. Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia.Katika Maonesho haya Kikundi cha HOT kiliweza kujinyakulia ushindi wa Tatu katika kundi la Washiriki wa Kimataifa ikitanguliwa na Kenya ambayo ilikuwa ya Kwanza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya Pili. Kikundi hiki kilikabidhiwa Kikombe na Mhe. Mhe. Michael Chilufya Sata, Rais wa Jamhuri ya Zambia siku ya Jumamosi tarehe 30 Juni 2012, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho. Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unatoa PONGEZI NYINGI KWA KIKUNDI HICHO











No comments: