Wednesday, June 20, 2012

Marehemu Willy Edward aagwa leo viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar

 Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbali mbali vya Habari hapa nchini wakijiandaa kushusha jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo,Marehemu Willy Edward Ogunde aliefariki dunia mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.Shughuli ya kuaga Mwili wa Marehemu Willy imefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar na baadae ikafuatia safari ya kwenda Nyumbani kwao Mara kwa Mazishi.
 Mchungaji akiongoza ibada ya Kuaga Mwili wa Marehemu Willy Edward leo.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini,Absalom Kibanda akisoma historia fupi ya Marehemu Willy Edward wakati wa Kuaga mwili wake leo kwenye Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe akizungumza kwenye shughuli hiyo ya kuaga Mwili wa Marehemu Willy Edward.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba akitoa neno kwa wafiwa wakari wa shughuli ya Kuaga mwili wa Marehe Willy Edward leo.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginald Mengi akimpa pole Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts ambao ni Wachapishaji wa Magazeti ya Jambo Leo,Juma Pinto wakati wa Shughuli ya Kuaga mwili wa Marehemu Willy Edward ambaye alikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Jambo leo,iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginald Mengi akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward ambaye alikuwa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo aliefariki ghafla huko mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe akitoa heshima zake.
Bw. Athuma Hamis akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward ambaye alikuwa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo aliefariki ghafla huko mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.Hafla hii ya kuaga imefanyika mchana huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar.
Mwili wa Willy Edward ukiwekwa katika sehemu yake tayari ibada ya kuaga.
Waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho.
Ankal akiwa na Mwanalibeneke Francis Godwin
Ankal akisabahiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginald Mengi.
Ankal akiwa katika mazungumzo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo Mbali mbali vya habari nchini wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini,Absalom Kibanda akibadirishana mawazo na Mkuu wa Masoko wa Benki ya NMB,Iman Kajura.
Mwili ukipakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya Mara kwa Mazishi.
Waombolezaji.

No comments: