Thursday, May 24, 2012

Hafla ya siku ya Africa yafana sana Jijini Washington DC

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akiwasili kwenye ukumbi wa J.W Marriot Mjini DC kuhudhuria dhifa ya chakula cha usiku kusherehekea siku ya Africa tarehe 23 Mei 2012. Anayemuongoza Balozi ni flag bearer model wa Kitanzania Hamisa au Miss Temeke ambaye alibuni vazi la kitanzania mahsusi kwa shughuli hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dkt Asha-Rose Migiro akihutubia kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya J.W Marriott jijini Washington DC Marekani leo tarehe 23 Mei 2012.
Mhe. Balozi Maajar akifuatilia salamu za Mhe. Kalonzo Musyoka, Makamu wa Rais wa Kenya alizotoa kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya J.W Marriott jijini Washington DC Marekani leo tarehe 23 Mei 2012.
Mkuu wa Utawala Ubalozini Mrs. Lily Munanka akiwa na mgeni wa Tanzania kwenye hafla hiyo Rais wa gazeti la Washington Times Bw. Thom McDevitt pamoja wakifuatilia salamu za Dkt Asha-Rose Migiro alizotoa kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya J.W Marriott jijini Washington DC Marekani leo tarehe 23 Mei 2012.
Meza ya Tanzania ikiwa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania na wageni wao, Kulia ni Brg. General Maganga, Mwambata Jeshi; Mr. Felix Ndunguru na Jesuit Temba, maafisa wawili kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii waliopo Washington DC kuhudhuria mikutano mbalimbali kuhusu uhifadhi wa masalia ya binadamu wa kale yaliyovumbuliwa Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dkt Asha-Rose Migiro akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar
Maafisa wa ubalozi kwenye picha za pamoja na Dkt Asha-Rose Migiro na Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar kwenye hafla hiyo ya chakua cha usiku.

No comments: