Thursday, May 10, 2012

Hafla ya Bia ya Kilimanjaro Kutangaza udhamini Mkuu kwa Timu ya Taifa (Taifa Stars) yafana sana jijini dar

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodger Tenga (kushoto) akibadilishana Mkataba wa Udhamini wa Bia ya Kilimanjaro kwa Timu ya Taifa "Taifa Stars" na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodger Tenga (pili kushoto waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (pili kulia waliokaa) wakisaini Mkataba wa Udhamini wa Bia ya Kilimanjaro kwa Timu ya Taifa "Taifa Stars" wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.Wanaoshuhudia ni viongozi mbali mbali wa TFF na Kampuni ya Bia Tanzania.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo (kulia waliokaa) na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na hadhi za Wachezaji,Alex Mgongolwa wakisaini mkataba huo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akipiga mpira kuashiria kuwa sasa udhamini umekalika kwa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche akitoa hotuba yake fupi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodger Tenga akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania kwa kuweza kuidhamini timu ya Taifa "Taifa Stars" kupitia Bia yake ya Kilimanjaro,wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akitoa maelezo mafupi ya Udhamini huo kwa wageni mbali mbali waliofika ukumbini hapo.
MC Ephraim Kibonde akiongoza shughuli hiyo.
Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo,Loenard Thadeo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Hivi Ndivyo Mambo yalivyokuwa wakati wa hafla fupi iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Kibo,ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.

No comments: