Tuesday, March 20, 2012

Sherehe za Kusimikwa Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara leo


 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,kabla ya safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera wakati wakielekea kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero leo.Watatu Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi (kushoto) na Mkewe Mama Sitti Mwinyi (katikati) wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa (kulia) kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo,Muhashamu Salitaris Melchior Libena iliyofanyika leo Ifakara,Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.
 Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akiongoza ibada yake ya kwanza akiwa ni Askofu wa Jimbo Jipya la Ifakara mara baada ya kusimikwa leo.
 Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa Viongozi wa Serikali waliohudhulia Sherehe hizo za kusimikwa kwake leo.
Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa wageni mbali mbali waliohudhulia Sherehe hiyo,wakiwemo waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa salamu kwa wakristo waliofika kwenye Sherehe hizo leo,ambapo ameliomba Kanisa Katoliki kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akihutubia kwenye Sherehe hizo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo mara baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika leo Ifakara,Mkoani Morogoro.
Mh. Lowassa akibadirishana mawazo na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Ifakara.

Mh. Lowassa akizungumza na Mmoja wa wananchi wa Mji wa Ifakara.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono.

No comments: