Monday, March 19, 2012

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya watimiza miaka 10 leo

  Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akihutubia leo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es salaam leo, huku Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Mh Frederick Sumaye wakiwa miongoni wa wageni mashuhuri walkioalikwa na kutunukiwa tuzo kwa juhudi zao zilizofanikisha kuanza na kushamiri kwa NHIF
 Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa Tuzo ya Kuenzi mchango wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Bima ya Afya katika uzinduzi wa  maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo uziliofanyika kwenye ofisi kuu ya mfuko, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Machi 19, 2012.Kushoto ni Waziri Mkuu, Frederick Sumaye ambaye pia alipewe tuzo hiyo
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa  (katikati) na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka  10 ya Mfuko wa Bima ya Afya kwenye  ofisi kuu ya mfuko huo barabara ya Kilwa  jijini Dar es salaam 

 Brass Band ya Polisi ikitumbuiza
 Ankal akiwa miongoni mwa Mashujaa wa NHIF waliotunukiwa tuzo leo

 Da' Faraja Kihongole wa Channel 10 akiwa na tuzo yake, akiwa na mwanahabari mwingine mkongwe Joyce Bazir ambaye pia alitunukiwa tuzo kwa kusaidia kueneza elimu kwa umma juu ya NHIF
Ankal baada ya kupokea tuzo yake

 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw Emmanuel Humba akiongea
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Lucy Nkya akihutubia
Waziri Mkuu akitembezwa kuangalia shughuli za NHIF. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Saidi Meck Sadik 
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Mh Wilson Mukama akipokea tuzo kwa mchango wake kufanikisha utendaji wa NHIF



Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, akifurahia tuzo maalum aliyozawadiwa baada ya kuwa msimamizi wa karibu na wa moja kwa moja wa mfuko huo katika miaka ya mwanzo hasa wakati makundi mengi yalikuwa yanapinga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akizindua kitabu cha taarifa za mfuko huo vijijini zilizokusanywa na wanahabari katika mikoa mbalimbali nchini. Kushoto ni Ofisa Habari na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakionesha vitabu viwili vilivyozinduliwa jana kikiwemo cha kuelezea maendeleo ya mfuko huo. Watumishi hao walishiriki kuhariri vitabu hivyo.
 Baadhi ya viongozi na watumishi wa mfuko huo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkapa
 Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wilson Mukama akipokea tuzo
 Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya NHIF, Profesa  Lucian Msambichaka akipatiwa tuzo na Mizengo Pinda
 Rais mstaafu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Mjumbe mstaafu wa Bodi ya NHIF, Margareth Sitta akipatiwa Tuzo
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema (kulia)  alikuwa ni miongoni wa viongozi waalikwa.
 Mmiliki wa Blog maarufu ya Michuzi, Muhidin Issa Michuzi, akipatiwa tuzo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya baada ya kuwa mmoja wa mashujaa waliosaidia mfuko huo kusonga mbele
                 Michuzi akionesha tuzo hiyo. 
 Faraja Kihongole wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya kwa kutambua mchango wa kihabari wa kuendeleza mfuko huo
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF, Deogratias Ntukamazina (kushoto) akipokea tuzo kwa kuendeleza vizuri mfuko huo

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya (kushoto) akimkabidhi tuzo maalum, Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Emmanuel Humba kwa kutambua mchango wake mkubwa ikiwemo kutokata tamaa alipokuwa akishambuliwa na wadau waliokuwa wakipinga kuanzishwa kwa mfuko huo.

 Ntukamazina (kushoto akipongezana na Humba baada ya kukabidhiwa tuzo
                                 Picha ya pamoja ya mashujaa wa mfuko huo waliokabidhiwa tuzo
 Wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini, wakipata maelezo kuhusu mfumo wa kisasa wa kuhifadhi mafaili ya wateja wa NHIF
 Wageni waalikwa wakioneshwa jinsi mafaili yalivyopanwa kwa mpangilio mzuri 
 Wageni waalikwa wakiangalia mafaili yanayoandaliwa kutunzwa kwa njia ya kisasa
                     Mafaili yakipangwa vizuri ili yahifadhiwe kisasa zaidi 

1 comment:

Anonymous said...

Congrats NHIF for Ten years Anniversary.
Mnafanya kazi nzuri sana japo kuna changamoto nyingi.Tunawaomba mzidi kuboresha huduma.Tunajivunia kuwa na Mfuko huu.Kwani kwa kadi ya NHIF nina uhakika wa matibabu mimi na familia yangu bila wasiwasi wowote.
Mungu awabariki