Sunday, March 11, 2012

Fainali za Safari Lager Nyama Choma jijini Dar zafana sana,Kisuma Bar waibuka kidedeaaa

Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma,Bw. Said Mbweche kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni (mwenye suti nyeusi) akizungumza machache kabla ya kuanza kutoa zawadi wa washindi mbali mbali wa Mashindano hayo yaliyofanyika leo na kufana sana kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni.Wengine Pichani ni wakuu wa idara ya Masoko ya TBL,Majaji wa Mashindano hayo (mwenye mavazi meupe) pamoja na Wadau wa Safari Lager.
Nyama ikiwa jikoni.
Nyama ikiandaliwa tayari kwa kwenda kwa wateja waliohudhulia fainali hizo za Safari Lager Nyama Choma.
Nyama ikiendele kuiva jikoni.
Muwakilishi wa Bar ya Kisuma ambao ndio Washindi wa Kwanza wa Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma jijini Dar es Salaam,Bw. Kavishe akipokea zawadi yake ya fedha taslim kiasi cha sh. Mil. 1 kutoka kwa Mgeni Rasmi,Bw. Said Mbweche.
Muwakilishi wa Fyatanga Bar ambao ni washindi wa Pili akifurahia nafasi aliyoipata.
Muwakilishi wa Meeda Bar.
Muwakilishi wa Play Time Bar akichukua zawadi yake ya kushika nafasi ya tano.
Mgeni Rasmi katika Fainali za Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma,Bw. Said Mbweche kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni (mwenye suti nyeusi) akizungumza machache kabla ya kuanza kutoa zawadi wa washindi mbali mbali wa Mashindano hayo yaliyofanyika leo na kufana sana kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo na Kushoto ni Meneja Mauzo wa TBL,Flavian Ngole.
Furaha ya Ushindi kwa Wadau wa Kisuma Bar.
Sarakasi pia zilikuwepo wakati wa kushangilia ushindi.
Muhudumu akiburudishwa wateja wake kwa kuzecha kiduku.
Wadau wa TBL.

No comments: