Monday, January 9, 2012

NSSF kukamirisha Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni

 Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufulli akihutubia leo wakati wa hafla ya utiliaji wa saini wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unatarajiwa kuanza siku yeyote kuanzia hivi sasa leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkataba huo umesainiwa baina ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Wakandarasi kutoka nchini China ambao ni CHINA RAILWAY JIANGCHANG ENGINEERING CO. (T) LTD na MAJOR BRIDGE ENGINEERING CO. LTD.
 Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla hiyo leo ambapo ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuomba kazi za ujenzi huo wa mradi wa daraja la Kigamboni.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akihutubia katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau akifafanua jambo wakati wa kutoa hotuba yake juu ya mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambao utagharimu kiasi cha sh. Bilioni 214.6 na utachukua muda wa miezi 36.
 Mtaalamu wa Ujenzi wa Madaraja kutoka nchini Misri,Eng. Shwaibu akitoa maelekezo ya namna ujenzi huo utakavyokuwa.
 Mtendaji Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale akitoa ufafanuzi wa namna waliovyoweza kufanya utafiti wa namna mradi huo utakavyofanyika na mpaka kufikia kumalizika.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau ( wa pili kushoto) akisaini vitabu vya mkataba wa mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Mkurugenzi  Mkuu wa Kampuni ya ukandarasi ya China Railway Jiangchang Engineering,Bw. Shi Yuan (pili kulia) na Muwakilishi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Major Bridge Engineering,Bw. Zhou Yiqiao kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau (kushoto) akibabadilirishana vitabu vya mkataba wa mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Mkurugenzi  Mkuu wa Kampuni ya ukandarasi ya China Railway Jiangchang Engineering,Bw. Shi Yuan mara baada ya kusaini leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufulli,Waziri wa kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Sadick,Balozi wa Misri nnchini.
Baadhi wa Wadau Mbali mbali wakiwa kwenye hafla hiyo,wakiendelea kufuatilia kwa makini taratibu zilizokuwa zikiendelea hapo.
Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufulli akibadirishana mawazo na Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka.
Mh. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari.
Picha ya mfano wa Daraja hilo la Kigamboni.

4 comments:

JUSTICE FOR ALL LEGAL AID CENTRE said...

Afadhali hawata (PIGA MBIZI) tena.

Anonymous said...

vipi meli zitapita au litakua lifunguka kati n ihope they not goin to charge people to pass throughvu

Anonymous said...

wazo zuri sana becouse im sure there is innocent people in prison simply becouse they cant afford a solicitor o a lawyer.Nakuunga mkono kwa wazo lako hili ni zuri sana

Anonymous said...

Kwani watapita bure?