Sunday, January 1, 2012

Maelfu wajitokeza katika mazishi ya Mtangazaji wa BBC, marehemu John Ngahyoma leo

Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa pole kwa wafiwa wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji wa BBC marehemu, John Ngahyoma wakati wa mazishi yake yalioyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Kaka wa Marehemu, Ngalimecha Ngahyoma akizungumza kwa niaba ya familia baada ya mazishi.
Mkurugenzi wa ITV na Radio One, Joyce Mhaville akitoa salamu za pole.
Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Sport FM cha Dodoma, Abdallah Majura akitoa pole kwa wafiwa wakati wa mazishi.
Mkurugenzi wa Under the Same Sun, Vicky Mtetema akitoa pole kwa wafiuwa wakati wa mazishi.
David Eric Nampesya wa BBC akitoa pole kwa familia ya marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa mfanyakazi mwenzake, marehemu John Ngahyoma.
Faidh Ngahyoma (katikati) ambaye ni mjane wa aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la BBC, marehemu, John Ngahyoma akiwa na baadhi ya ndugu wa karibu wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Faidh Ngahyoma ambaye ni mjane wa aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la BBC, marehemu John Ngahyoma akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Sport FM cha Dodoma, Abdallah Majura akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu John Ngahyoma wakati wa mazishi yake leo.
Baadhi ya wafanyakazi wenzake wakiwe mashada ya maua.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

1 comment:

Anonymous said...

RIP JOHN NGAHYOMA MCHANGO WAKO NI MKUBWA SANA KATIKA JAMII YA TANZANIA. WAHUSIKA KAMA ITV NA BBC MSIMSAHAU MJANE NA WATOTO WA MAREHEMU KWANI NI WADOGO SANA MUENZINI KWA KUITUNZA FAMILIA YAKE