Sunday, October 23, 2011

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technologia Mh, Charles Kitwanga na Kampuni ya Airtel wafanya ziara mkoani Tanga

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Chiku Gallawa alipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni na kufanya nae mazungumzo mafupi wakati wa ziara yake mkoani humo. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Chiku Gallawa akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya aliekuwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga (hayupo pichani),ikiwa ni ziara ya kutembelea mkoa wa Tanga na kutathmini hali ya Mawasiliano ya simu za mkonini na jinsi ya kuyaboresha katika mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Kwa Mkole kilichopo kwenye kata ya Kizari,Wilaya ya Korogwe Vijijini ikiwa ni sehemu ya Ziara yake katika mkoa wa Tanga.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga akiwahutubia wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kwa Mkole ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha mawasiliano ya simu na kuwaambia kuwa sasa hizi mawasiliano yatapatikana kwa kila mmoja na mahala popote atakapokuwepo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia kujionea hali ya mawasiliano vijijini na kuangalia namna ya kuboresha huduma hiyo,akiwaeleza wanakijiji hao hali itakavyokuwa.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akijumuika na wanakijiji katika hao wakati Mh. Naibu Waziri akizungumza nao.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" (kulia) akimuonyesha kitu Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh. Charles Kitwanga wakati walipokuwa kwenye kijiji cha Kijango Magoma wilayani Korogwe vijijini hivi karibuni.
Wananchi wakimsikiliza Mh. Naibu Waziri wa Mawasiliano.
Safari ya Kuingia Korogwe Vijijini.

No comments: