Wednesday, September 7, 2011

WANAFUNZI WA KITANZANIA WASOMAO CHUO KIKUU LUMUMBA,MOSCOW-URUSI WAPEPERUSHA VYEMA BENDERA YA TAIFA KATIKA SOKA NCHINI URUSI.

Wanafunzi wa kitanzania wanasoma katika chuo kikuu cha urafiki (Lumumba) mji wa Moscow nchini Urusi wamefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya taifa katika medani ya soka katika michuano ya kombe la dunia chuoni hapo baada ya kushika nafasi ya pili katika mchezo wa mkali wa fainali dhidi ya wapinzani wao wakubwa Ivory Coast iliyopata ushindi wabao 1-0 kwa njia ya penalti iliyotolewa na mwamuzi katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.


Tanzania ambayo ilionyesha kandanda safi ilionekana kutokuwa na bahati siku hiyo kwani ilikosa magoli mengi ambayo yangeweza kubadili matokeo zaidi.


Michuano hiyo ambayo hujumuisha karibu nchi 20 zikiwemo zile zinazotamba kwa soka Afrika kama Nigeria ambayo safari yao ya mwisho ilikuwa kwa watanzania katika hatua ya robo fainali kwa kufungwa 2-1,na kuwatoa walatino katika pambano la nusu fainali kwa bao 2-1.Nafasi ya 3 ni Guinnea Bissau na 4 ni Walatino.

 Katibu wa michezo na utamaduni wa wanafunzi wa kitanzania ambaye pia ni mchezaji wa timu hiyo Mahamoud Mbarouk akiwa na zawadi ya kombe na medali mara baada kukabidhiwa na mkuu wa chuo.
 Beki mahiri wa timu ya Tanzania Robert akifurahia zawadi ya kombe baada ya mchezo.
 Wachezaji waTanzania wakiwa na rais  wao Mh.Rashidi Mohamed Kidirsha mwenye sweta la pundamilia akifuatiwa mdau Selemani Ditopile mwenye koti jeusi wakifurahia kombe.
 Kutoka kulia ni mdau wa soka wa kitanzania Nassoro Omary akiwa katika picha ya pamoja na bwana Rashidi Kidirisha,akifuatiwa na Mahmoud Mbarouk na mwisho ni bwana Octavian Nyalali.
 Kutoka kushoto ni naibu katibu wa wanafunzi wa kitanzania Mh:Octavian Nyalali,Mahamoud Mbarouk pamoja na mwenyekiti wa wanafunzi hao Mh:Rashidi Kidirisha wakiwa na zawadi zao.
 Mzee wa kuhamasisha mwanzo mwisho Yahya Mohamed mwenye koti jeusi akiwa na  na wachezaji  baada ya kukabidhiwa kombe.Koti la kijivuni mdau Alamsi Issa.
 Wachezaji,wadau na viongozi wa timu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mkuu wa chuo hicho bw.Filipov mara baada ya kuwakabidhi kombe hilo.
 Nahodha wa timu ya Tanzania Mapigano Nduhilubisa akipokea zawadi ya kombe kutoka kwa mkuu wa chuo.
 Juu na chini ni jukwaa la watanzania wakiwa uwanjani huku wakifuatilia kwa makini pambano hilo la fainali.
 Bongo fans

Kikosi cha Tanzania kikiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri wa michezo wa wanafunzi wa kitanzania chuoni hapo Bw.Zakayo (Black Rooney) mwenye fulana nyeusi wa kwanza kushoto waliochuchuma.
Timu ya Tanzania (Taifa Stars) kulia wakiwa na wapinzani wao Ivory Coast kabla ya kuanza kwa pambano hilo fainali.

1 comment:

Anonymous said...

Bendera ya Tanzania imeshikwa juu chini!!!!!!!!!! Upande wa mlingoti (yaani kule kwenye utepe mweupe na kamba za kushikia kwenye mlingoti) mistari ya black and yellow inaanza chini kuelekea juu na sio juu kuelekea chini kama kwenye picha. Poor Tanzanians after 47 years of using this flag bado hatujui jinsi ya kuishika.