Monday, August 8, 2011

libeneke la wese jijini dar leo


Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwenye kituo cha Mafuta cha GBP pale sinza Mapambano kutokana na vituo vingine vya mafuta kutofanya biashara hiyo kwa kugomea punguzo la bei lililopangwa na Serikali hivi karibuni.Kituo hiki ndicho kituo pekee kilichokuwa kikiuza mafuta kwa leo baada ya vituo kama vya BigBon TSN kuishiwa mafuta kutokana na uwingi wa watu wanaohitaji matuta kwa matumizi mbalimbali.hali hii imepelekea msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya sinza mpaka kufikia kufungana na kushindwa kutembea kwa magari kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Mmoja wa Waendesha pikipiki maarufu kama Boda Boda ambaye alifanikiwa kupata mafuta baada ya mshike mshike ya nguvu akijiandaa kupakia mafuta hayo kwenye usafiri wake tayari kwa matumizi ya bajeti kama alivyokuwa akiongea mwenyewe pindi mwenzie huyo alieshika vidumu vitupu alipoomba kuuziwa dumu moja hata kwa bei ya juu.
Ulifika wakati huduma ikasitishwa kutokana na vurugu zilizokuwa zikiendelea kituoni hapo.
Hakuna uchakachuzi wa foleni hapa,maana kila mtu alikuwa makini katika hilo.
Jamaa wa Boda boda akimimina mafuta aliyouziwa na mwenzake.
Mdau akifurahi kwa kupata mafuna na kusema afadhali ataweza fika nyumbani kwake.
huduma imesitishwa mpaka utaratibu ufuatwe.
hii ni moja ya foleni katika moja ya pampu za kituo hicho.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika barabara ya Sinza wakati magari hayo yakiingia kwenye kituo cha mafuta cha GBP.
hapa ni mwenye kuwahi ndio mwenye kupata.
Watu wamepanga foleni tokea saa nane mchana na bado hawajapata huduma.
Jamaa kafanikiwa kupata dumu zote hizo na ndio anajiandaa kuondoka.
Wengine wameamua kukaa chini kutokana na kusimama kwa muda mrefu.
Kikao cha Dharula
Bango la bei ya Mafuta.

No comments: