Wednesday, August 3, 2011

baadhi ya wauza mafuta waitingishia kiberiti serikali

"....Kaka samahani wese leo hatuuzi
Kaka vipi wese leo??
Wafanyakazi wako likizo
Msululu sheli ya BP ya mtaa wa makunganya
Mdau kaambulia lita tano za kumfikisha nyumbani
Foleni kwenye kila kituo kinachouza mafuta leo
Mdau kabahatika kujaza fulltenki
"....Ebwana dah! wese ndio limekata saa hivi..."
"....Sasa kama wese hamna nikutilie maji??"
"Ngoma ikemata hiyo, si unaona mwenyewe braza..?

Sheli ya Gapco barabara ya Sokoine yaokoa jahazi na bei mpya
 "...We kaka si unaona kamba hiyo tumefunga kabisa hakuna wese...?
Ah, angalau kaambulia
"Hapa tukiomba mpira wa kufyonzea itakuwa taabu, maana jamaa wana hasira hao..."
Jaza twende
Samahani anko afande. nimekula boda sababu nawahi wese nasikia Buguruni yanatoka...

 Simba Oil ya Tabata mambo mswano...
 Na Lukwangule
LEO huenda ikawa ndio siku nyingine ya majaribio kwa serikali ya Tanzania, ambapo watu wa mafuta baada ya kupewa ujiko wa kupandishwa kwa bei ya mafuta ya taa wakapandisha hata bila maelekezo ya serikali, wameamua kuivimbia serikali kwa staili ya kusema tuone.

Staili hiyo ya kuacha kuuza mafuta baada ya serikali kutoa bei elekezi inaonesha kiburi kilichojengwa na wafanyabiashara wa mafuta nchini.

Baadhi ya vituo katika miji ya kibiashara nchini, Dar es salaam,Morogoro, Iringa, Mbeya vimekataa kutoa huduma kwanza kwa visingizio vya umeme na baadaye kwa dai kuwa wana akiba ya mafuta ya zamani.
Vituo vya mafuta vilivyokuwa vikiendelea na utoaji wa mafuta vilijikuta vikielemewa.

Kutokana na mazingira yaliyopo ni aibu kwa serikali kuchezewa namna hii, serikali ni lazima iwe serikali.
Watu waligoma Muhimbili, wanajeshi waliingia, watu waligoma kuongoza ndege , wanajeshi waliingia nadhani Balele alikuwa mmoja wa wtau waliotumika kuweka mambo sawa katika anga la Tanzania.

Kutokana na hoja yangu hiyo nasema kwanini wanajeshi wasifike katiika vituo hivi wakachukua leseni za hawa jamaa, wakaangalia kama kweli mafuta yapo au hayapo au jenereta halifanyikazi au linafanyakazi na kwanini liharibike siku ya kushusha kwa bei kisha wauze mafuta hayo na fedha iingie Hazina .

Watu hawa wangelikuwa kwa kagame sasa hivi walichakula risasi au wako lupango wakisubiri utaratibu mwingine. Tunatatizo la umeme hawawezi kutuletea kizaazaa kingine hapa hawa ni wauaji.
hebu fikiria huyu Mfanyakazi katika kituo cha mafuta cha BP kilichopo Mwanjelwa jijini Mbeya anavyosema.. eti Serikali haiwezi kushindana na wafanyabiashara na kwamba lazima mafuta yauzwe kulingana na bei wanayoitaka wafanyabiashara na si serikali.

"Mimi sifaidiki na lolote kwa kukosekana kwa mafuta lakini nynyi ndio mtakaoathirika kwa kuwa leo hamtafanya kazi yoyote"

Hivi hawa ni nani hasa? Wanatoka wanakimbilia wizarani eti hii imekuja ghafla! Ghafla? Ghafla ya nani? Watu walimuuliza Waziri Mkuu mbona umetoa tozo na mafuta yako juu akasema subirini jamani zinahitajika lojistiki. Hawa nani lojistiki zinapokuwa sawa wanasema si sawa? 

Wengi wa wenye makampuni haya ni wageni tu!
kwanini tunachezewa chezewa hivi?Mtu anauza mafuta kwa sh 5000 kwa makusudi kabisa na tunamwangalia.

No comments: