Saturday, July 16, 2011

Tamasha la Kilimanjaro Jivunie Utanzania lafana sana leo

 Meneja wa Bia  ya Kilimanjaro,George Kavishe (pili kulia) akiwa na Meneja Mauzo wa Kampini ya Bia Tanzania (TBL),Flavian Ngole (tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya InterGrated,Fred Nthiga wakati wakijiandaa kwa maandamano ya Tamasha la Kilimanjaro Jivunie Utanzania yaliyoanzia kwenye Kijiji cha Makumbusho na kumalizikia kwenye viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar es Salaam leo. 
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (kulia) akiwa na Meneja Mauzo wa TBL,Flavian Ngole wakiongoza maandamano ya Tamasha la Kilimanjaro Jivunie Utanzania yaliyoanzia kwenye Kijiji cha Makumbusho na kumalizikia kwenye viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar es Salaam leo. 
 Gari lililokuwa limewapakia washehereshaji likikatiza mitaa ya kijitonyama leo.
 Maandamano yakiendelea kuelekea viwanja vya Posta,Kijitonyama.
 Gwaride la nguvu lilipigwa leo. 
 Wadada wakiwa na bendera zao zenye ujumbe usemao "JIVUNIE UTANZANIA"
 Msafara wa Magari ya TBL.
 Msafara wa Pikipiki za TBL.
Wasanii kutoka kundi GYT wakiigiza kama wanamuziki wa zamani  wakitumbuiza wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Jivunie Utanzania linalofanyika katika Viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar es Salaam mchana huu.
 Wasanii wa kikundi cha GYT, Tiamaji na  Lina wakifanya vitu vyao wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Jivunie Utanzania linalofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam mchana huu.
Msanii mwenye asili ya Kimasai akitoa burudani wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Jivunie Utanzania linalofanyika kwenye Viwanja wa Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mchana huu.
Vijana wa GYT wakiendelea kufanya mambo yao.

No comments: