Friday, July 15, 2011

Yusuf Kikwete na Mariam Ombaka walivyomeremeta bagamoyo

Rais jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt Mohammed Gharib Bilal, wakiongozana katika Uwanja vya Ikulu Ndogo Bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake na rais Kikwete, Yusuf Kikwete, iliyofungwa leo mchana katika uwanja huo na kuhudhuriwa na mbalimbali pamoja na wake za viongozi.
Bwana harusi, Yusuf Kikwete akiongozana na wapambe wake wakati wakiingia katika uwanja huo kwa ajili ya kufunga ndoa.
Sheikh, akitoa mawaidha baada ya bwana harusi kufungishwa ndoa.
Bwana Harusi, Yusuf Kikwete , akifungishwa ndoa na Sheikh. Aliyemshikia mike ni kaka yake Mohamed Kikwete
Bwana Harusi Yusuf na waumini wa dini ya Kiislamu wakiomba dua baada ya tendo la kufungishwa ndoa.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Bilala, wakiwa katika meza kuu kwenye Sherehe hiyo iliyofanyika Bagamoyo leo.
Rais jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete na Bwana na Bi Harusi.
 Rais Jakaya akisalimiana na Mudhihir Mudhihir, walipokutana katika sherehe hiyo.
Miraji Kikwete, naye hakuwa mbali katika kunasa matukio, hapa alikuwa akimpiga picha baba yake mdogo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete na Bwana  Yusuf Kkikwete na Bi Harusi Mariam Ombaka.
Bwana harusi akipiga picha ya kumbukumbu ya pamoja na wake za viongozi.
Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama Asha Bilal, wakati wakiwa katika sherehe hiyo ya ndoa ya mdogo wake na Rais Jakaya Kikwete, Yusuph Kikwete leo mjini Bagamoyo.
Bwana Harusi, Yusuph Kikwete akiwa na mkewe Mariam Ombaka, baada ya kufungishwa ndoa.


No comments: