Tuesday, July 26, 2011

Jimmy David Ngonya 'Gorberchev' aagwa leo jijini Dar

 Mwenyekiti mstaafu wa Yanga Imani Mahugila Madega (shati jeupe), Constantine Marigo (shoto) Mussa Mtulya wa Empress na mdau wakiwa katika kanisa la Hospitali ya Muhimbili kumuaga Katibu Mkuu wa zamani wa Simba SC Jimmy David Ngonya  'Gorbachev' kabla mwili wake haujasafirishwa kuelekea kijijini kwake Lutengano, Tukuyu, mkoani Mbeya kwa mazishi
 Da'Asha Baraka akiongea na wachezaji wa zamani wa Simba Mtemi Ramadhani (wa tatu kushoto) na Abbas Kuka (wa pili kulia) wakati wa miba wa Ngonya
 sehemu ya waombolezaji kanisani
 Viongozi wa sekta mbalimbali walikuwepo
 Viongozi na wafanyakazi wa PPF walijitokeza kwa wingi. PPF ni mtoto wa shirika la Bima ambako Marehemu Ngonya alikuwa kiongozi katika mafunzo na utawala ambapo wafanyakazi wengi wa Bima na PPF alifunza ama aliajiri yeye
 Evans Aveva akiwakilisha Friends of Simba na wadau wengine

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini Bw. Israel Kamuzora akitoa neno kwa niaba ya sekta ya Bima nchini
 "...Buriani David. Hatuamini kwamba umekwenda....!" Mzee anasema kwa huzuni
 Wadau toka kila pembe ya jiji
 Waombolezaji wamefurika kanisani
 Waombolezaji
 Familia ya marehemu
 Ndugu na jamaa wa marehemu
 Waombolezaji
 Mzee amlilia JD Ngonya
 Wadau wa PPF na kwengineko
 Waombolezaji
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio akitoa rambirambi za mfuko huo
Salamu toka Chuo cha Uanamaji (TMI) zinawasilishwa na  Afande Sande Ligate
 wadau msibani
 Msemaji wa Simba Sc Ezekiel Kamwaga akitoa rambirambi za wekundu wa Msimbazi
 Muddy Pizzaro akiwakilisha Break Point na SingaSinga
 salaam za Mfuko wa Bima ya Afya
 Profesa Esther Mwaikambo akitoa salamu za rambirambi
 Wana Lutengano wakiombolea
 Mwana Lutengano akimsindikiza mfiwa
 Wadau msibani
 Taswira za msibani
 Imani Madega na wadau wa Simba na Yanga msibani
 Foleni ya kwenda kuaga mwili wa marehemu
 Waombolezaji
 kanisani

 Bw. David Mattaka kashika tama akifuatiwa na Bw. Israel Kamuzora na Bw. William Erio
Mwana mkubwa wa marehemu akitoa shukurani

4 comments:

Anonymous said...

mungu amuweke mahala pema alikuwa ni kiongozi imara asiye tetereka henzi za huai wake.
said john

Rama Abeid said...

Kwa hakika mimi nikiwa mdau mkubwa wa Simba Sports Club bado hajatokea kiongozi mahiri ambaye alikuwa hababaishwi na watu uchwara na wenye kuitumia Simba kwa manufaa yao kama watu fulani hivi ambao walikuwa viongozi.

Ninaweza kumfananisha na Alhaj Aden Rage kwa sasa ambaye nae amekataa kata kata kuburuzwa na akina nanihii........ wanaotaka kuchota fedha za klabu kwa manufaa yao binafsi.

Kapumzike kwa amani Gorbachev Jimmy David Ngonya. TULIKUPENDA ila Mwenyezi Mungu AMEKUPENDA ZAIDI.

Rama Abeid

Anonymous said...

napenda nimrekebishe mwandishi huyo aliyeshikwa hapo akiangalia mwili wa mzee wetu si mjane wa marehemu bali ni mtoto wa marehemu ,naomba abadilishe kabla wenyewe hawajaona.plse

Anonymous said...

Kapumzike kwa amani baba. Kwako tumejifunza ukarimu, upendo, amani, msimamo na ushirikiano. Gwende ufike Mundu gwa Kyala.