Friday, July 29, 2011

BUNGENI DODOMA LEO

Naibu Spika Job Ndugai (wa pili kutoka mbele) akiingia bungeni leo kwaajili ya kuanza kikao cha thelathini na sita katika mkutano wa nne wa bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiongea jambo na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-MAGEUZI) David Kafulila (kushoto) leo katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa nne wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo hotuba iliyotolewa jana na Godbless Lema ambaye ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi.
Mbunge wa Bumbuli (CCM) January Makamba akimuuliza swali waziri wa Nishati na Madini kuwa Serikali inamapango gani wa kuendeleza mradi wa umeme katika kata ya Mgwashi leo katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa nne wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Maswa Mashariki (CHADEMA) Sylvester Kasulumbai akichangia hoja kuhusu kuhusu bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Bungeni leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Mtera (CCM) Livingstone Lusinde akitoa mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge wa kikao cha thelathini na tano kilichofanyika jana mjini Dodoma Jenista Mhagama (hayupo pichani) kuwa wabunge wate wakapimwe akili hii ni kutokana na matukio ya uvunjifu wa kanuni yanayotokea mara kwa mara ndani ya Bunge.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na Naibu waziri wake Balozi Khamis Kagasheki (kulia) wakiandika michango mbalimbali iliyokuwa inatolewa na wabunge kuhusu bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo leo kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Bungeni leo mjini Dodoma
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli (katikati) akifurahia jambo na Mbunge wa Vunjo (TLP) Augustino Mrema(kushoto) na Mchungaji Israel Natse (CHADEMA) (kulia) Mbunge wa Karatu kabla ya kuanza kwa kikao cha thelathini na sita katika mkutano wa nne wa bunge unaoendelea mjini Dodoma.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

No comments: