Matukio haya na yale sambamba na habari/picha za ziada za Globu ya Jamii
Wednesday, April 20, 2011
SHEREHE ZA MIAKA 38 YA OKINAWA GOJU RYU KARATE DO NCHINI TANZANIA
Kepteni mstaafu wa JWTZ Sensei Geoffrey Shoo ambaye ni Chiefanaki Instructor wa Okinawa Den Goju Ryu Arnis, Kali na Escrima ambaye pia ni mwanasheria akielezea historia ujio wa sanaa hii ya kujilinda katika dojo kongwe kuliko yote nchini usiku huu katika hekalu la kujilinda lililopo katika shule ya msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za miaka 38 ya dojo hili Sensei Geoffrey Shoo akimtambulisha Sensei Brighton Manyau (shoto) ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa kwanza wa muasisi wa Goju Ryu karate nchini hayati Namtambu Camara Bomani, akifuatiwa na Sensei Malekia, kiongozi mkuu wa Hekalu la Kujilinda Sensei Malekia akiwatambulisha Chief Instructors (Sensei) wapya waliopandishwa daraja usiku huu. Toka kulia ni Sensei Geoffrey Mbezi, Sensei Rashi Almasi na Sensei Ndaukile Amri Sensei Brighton Manyau akimvisha mkanda wa kijani mmoja wa vijana wanne waliopanda daraja toka mkanda mweupe Sensei Manyau akimpandisha daraja mwanafunzi kijana Sensei Manyau akimlisha keki Sensei Malekia Sensei Sawayaeli Geoffrey Shoo akipata keki ya sherehe Sensei Manyau akikata keki. Chini akimpandisha daraja Sensei Mbezi Sensei Malekia akieleza jambo Sensei Ndaukile Amri akipandishwa daraja
Masensei wakiwa na wanafunzi waliopandishwa daraja Sensei Malekia akiwa na vijana wadogo waliopanda daraja toka mkanda mweupe kwenda wa kijani Sensei Rashid Almasi akipandishwa daraja Juu na chini wana Goju Ryu na wageni wakisimama kimya dakika moja kumkumbuka hayati Adam Lusekelo, mmoja wa wanafunzi wa awali hapo dojo Producer wa muziki Ramal (kulia) akijiandaa kupiga kumite na mmoja wa wanafunzi waandamizi. Wadau toka kila fani ni wanafunzi katika dojo hili Vijana wengi wanashiriki katika dojo hili Ankal akiwa na masensei. Yeye pia kapitia mafunzo haya kwa miaka takriban 18 Kata ya Geki Sada Ichi Kata ya Geki Sada Nii Juu na chini ni namna ya kumdhibiti adui mwenye kisu Kisu hakifuagi dau mbele ya mwana Goju Ryu... labda - labda - uje na cha moto... Kinadada nao wamo kwa sana tu... Mgeni rasmi Sensei Brighton Manyau akiongoza wanafunzi na wageni waalikwa katika mnuso Wageni wakipatiwa mlo Bondia veterani Iraq Hudu naye alikuwepo Msosi wa nguvu
No comments:
Post a Comment