Thursday, April 28, 2011

Rais wa shirika la Under The Same Sun akiongea na watu wenye ulemavu wa ngozi leo

Rais wa Shirika la Kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi linalofahamika kwa jina la UNDER THE SAME SUN,Peter Ash akizungumza jiono ya leo na baadhi ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na wanahabari huku Mkurugenzi wa Shirika hilo hapa nchini,Vicky Ntetema akimsaidia kutafsiri kwa kiswahili ili kuwaelewesha wale wasiojua lugha la kiingereza.hii ni katika hafla ya mkutano na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Nyumbani Hotel,jijini Mwanza.Mkuu wa Wilaya ya Misungungwi,Mh. Mariam Lugairwa akizungumza katika mkutano huo jioni ya leo,ambapo aliwataka watu kujituma katika kufanya kazi ili kufanikiwa katika maisha na si kuweka dhana potofu ya kusema kwamba ili mtu afanikiwe kimaisha basi li lazima apate viungo vya albino.hii ni jioni ya leo katika hafla iliyoandaliwa na shirika la UNDER THE SAME SUN katika hoteli ya Nyumbani,jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoani Mwanza,Alfred Kapole akizungumza wakati akifungua mkutano huo jioni ya leo.
Maafisa wa Shirika la UNDER THE SAME SUN kutoka jijini Dar wakibandika baadi ya picha ukumbini hapo.
Watoto wenye ulemavu wa ngozi ambao walihudhulia hafla mkutano kati ya Shirika la UNDER THE SAME SUN na watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mwanalibeneke wa Libeneke la G. SENGO,Albert Sengo akiwa bize kuandika yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo.
Mwanachuo kutoka Chuo cha Mt. Augustine,Monalisa Juma akichangia mawazo katika mkutano huo.
Mkalimani wa Lugha ya Alama kwa ajili ya watu wasiosikia,Jonathan Livingston akiwatafsiria baadhi ya watu waliohudhulia katika mkutano huo ambao walikuwa hawasikii.
Mkutano ukiendelea.

Mama wa Mtoto afahamikaye kwa Jina la Manyashi (kushoto) akiwa pamoja na mumewe (kati) wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari waliohudhulia mkutano huo.
Mambo yakiendelea ndani ya ukumbi wa Nyumbani Hoteli jijini Mwanza leo.

No comments: