Friday, February 18, 2011

waathirika wa mabomu katika hifadhi ya muda uwanja wa UHURU jijini Dar

Baadhi ya wakazi wa Gongo la Mboto wakiwa wamejihifadhi kwa muda uwanja wa Uhuru jijini Dar wakati wa dharura ya mabomu
Mfanyakazi wa Red Cross akimtuliza mmoja ya watoto wengi waliopotezana na ndugu zao baada ya milipuko
Viongozi wa juu wa UVCCM wakiwafariji waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto
Mwenyekiti wa wa NCCR-MAGEUZI Mh. James Mbatia (shoto) na wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakiwafariji waathirika uwanja wa UHURU
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea wakati wa kuwafariji waathirika wa mabomu Gongo la Mboto alipotembelea uwanja wa UHURU. Amependekeza viongozi husika kuwajibika mara moja na pia katoa rai kwamba wakati umefika makambi ya jeshi yakatafutiwa mahali mbali na makaazi ya raia kwani tofauti na ilivyokuwa awali ambapo makambi yalionekana kuwa mbali na makaazi ya raia, hivi sasa miji imepanuka na makambi yamejikuta yako katikati ya uraiani. Ametoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuomba watanzania wasaidie kupunguza makali ya maisha kwa waathirika na machungu kwa wafiwa na majeruhi

No comments: