Saturday, January 20, 2018

SHIMIWI kutekeleza agizo la Makamu wa Rais

Uongozi mpya wa Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mara baada ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye hoteli ya Mount Uluguru mkoani Morogoro.


SHIRIKISHO la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), litatekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Tanzania Bara, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na mabonanza kila mwisho wa mwezi yatakayohusisha wachezajiw a michezo mbalimbali.

Moshi Makuka, Katibu Mkuu wa SHIMIWI, alisema wamekubaliana katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hivi karibu, ambapo wataanza na bonanza kubwa litakalofanyika Februari mwaka huu mkoani Dodoma, ambapo sasa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali zimeshahamia mkoani hapo.

“Hili bonanza litakuwa kubwa sana kwani ukiangalia tayari wizara, taasisi na Idara za serikali kwa asilimia kubwa zimeshahamia Dodoma, hivyo timu zianze kujiandaa na baada ya kukamilisha hili baadaye katika tarehe zitakazotangazwa tutafanya tena Jijini Dar es Salaam,” alisema Makuka.

Makamu wa Rais, mwaka jana alitoa agizo kufanyike mazoezi ya kila mwezi kwa kuhusisha wafanyakazi ili kujijengea afya zao. Michezo inayochezwa SHIMIWI ni pamoja na soka, netiboli, kuvuta kamba, baiskeli, karata, bao na draft (wanawake na wanaume).

Mbali na kuanza kwa mabonanza, pia Kamati hiyo ya Utendaji imeunda Kamati mbalimbali ikiwemo ya Habari na Mawasiliano ambayo itaongozwa na Itika Mwankenja (Mwenyekiti), Elias Malima (Katibu), huku wajumbe ni Bahati Mollel, Jane John, James Katubuka, David Kitila na Jessey John; kamati ya utendaji na nafasi zao ni Daniel Mwalusamba (Mwenyekiti), Ally Katembo (Makamu Mwenyekiti), Makuka (Katibu Mkuu), Alex Temba (Katibu Msaidizi), William Mkombozi (Mweka hazina), Frank Kibona (mweka hazina msaidizi) na wajumbe ni Appolo Kayungi, Damian Manembe, Seleman Kifyoga, Assumpta Mwilanga na Aloyce Ngonyani, huku wajumbe wa viti maalum ni Mariam Kihange na Mwajuma Kisengo.

Wanaounda Kamati ya Mipango ni Mwalusamba Mwenyekiti), Mkombozi (Katibu) na wajumbe ni Makuka, Ngonyani, Kihange na John Jambele; huku kamati ya Ufundi inaundwa na Kayungi (Mwenyekiti), Manembe (Katibu) na wajumbe ni Kisengo na Joyce Benjamin; Kamati ya Nidhamu wapo Katembo (Mwenyekiti), Temba (Katibu) na wajumbe ni Marcel Katemba na Mwilanga.

Kamati ya usajili itaongozwa na Temba (Mwenyekiti), Kibona (Katibu) na James Emmanuel (Mjumbe); nayo Sekretarieti ya Uendeshaji inaundwa na Kihange (mwenyekiti), Kifyoga (Katibu), na wajumbe ni Bahati Magambo, Buya Ndalija, Justo Mwandelile, Ahmed Chitagu, Peter Lihanjala, Gracia Kyelula, Peter Onono, Modesta Kaunda, Amina Kakozi, Ismail Ismail, Sophia Mkama na James Emmanuel.

Nayo Kamati ya Huduma za tiba itaongozwa na Joakim Mwaipaja (Mwenyekiti), Magreth Mtaki (Katibu), na Wajumbe ni Richard Yomba, Haji Masasi, Jafari Chikoko na Gration Kaizirege.

No comments: