Wednesday, December 7, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa serikali kwenda kuwatatulia wananchi matatizo yao na kuacha tabia ya kujichimbia mijini; https://youtu.be/z-g0fjHpuy8

SIMU.TV: Sakata la mifugo kuvamia sehemu za makazi limeingia mkoani Morogoro eneo la Kiegea na kusababisha taharuki baina ya wafugaji na wakazi wa eneo hilo; https://youtu.be/Q6h1ZeqAY0A

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme amezisimamisha kazi kamati za maji kata ya Ihumwa kwa sababu za ubadhirifu wa fedha; https://youtu.be/JC8ZWmC2qf0

SIMU.TV: Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi amesema licha ya kupatikana kwa maendeleo katika miaka 55 ya Uhuru bado tatizo la ubinafsi linaathiri maendeleo zaidi; https://youtu.be/6rsfejgbvSk

SIMU.TV: Rais Dkt John Magufuli leo amefanya mabadiliko madogo katika wizara mbalimbali na kuteua mkuu wa mkoa mmoja; https://youtu.be/QoI2Snv-RX0

SIMU.TV: Bidhaa za vyakula vilisindikwa na wajasiriamali wanawake vimeonekana kuwa kivutio kikubwa katika maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea hapa Dar Es salaam; https://youtu.be/UisAwDo50ZI  

SIMU.TV: Wataalamu wa biashara kutoka Tanzania na Rwanda wanajadiliana namna ya kuondoa vikwazo visivyokuwa kodi ili kuboresha ufanyaji wa biashara; https://youtu.be/xYofqpiOVKQ

SIMU.TV: Biashara imeendelea kuwa ngumu kwa ushirika wa viwanda vidogo Dar Es salaam baada ya kushuka kwa makusanyo ya fedha waliyojiwekea; https://youtu.be/Cv229RZypsg  

SIMU.TV: Shirikisho la mpira nchini TFF kupitia kamati ya masaa 24 limewaengua waamuzi Martin Saanya na wenzake watatu baada ya kuvurunda katika michezo ya mzunguko wa ligi uliopita; https://youtu.be/6inKxfpTPqw

SIMU.TV: Jumla ya nchi tano zitashiriki mashindano ya masumbwi ya riadha huku wadau mbalimbali pamoja na makampuni wakiombwa kujitokeza kudhamini mashindano hayo; https://youtu.be/WUv9v7nYIgQ

SIMU.TV: Makocha wanaofundisha soka la vijana chini ya miaka 14 wameridhishwa na viwango vinavyoonyeshwa na watoto hao na kuvitaka vilabu vya ligi kuu kuwa timu za watoto; https://youtu.be/9uMf-0qBoX4

No comments: