Friday, November 25, 2016

BALOZI DK ASHA ROSE MIGIRO ALIPOHUTUBIA KIKAO CHA JUMUIYA YA WAINGEREZA NA WATANZANIA – BTS

Picha na Habari za Freddy Macha, London 
Balozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia  jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS)  Jumamosi iliyopita. 
Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose.
Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania”  Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza wakazi hapa.
Wajumbe wa BTS wanaipenda Tanzania na kusimamia miradi tele kwa kujitolea bila hata senti moja. Mwaka 2015-2016 BTS imeendeleza mipango 46 ya maendeleo haya.
Mama Balozi alizungumza kifupi akisisitiza masuala muhimu ya maendeleo ya elimu, uongozi  mpya wa Rais John Magufuli unaosisitiza “Hapa Kazi Tu” katika kipindi cha mwaka mzima. Baada ya hapo alitumia muda mwingi kujibu maswali ya wajumbe. Aidha masuala yalijibiwa  au kupewa ahadi ya kufuatiliwa kivitendo. 

1-balozi-migiro-akihutubia-jumuiya-ya-watanzania-na-waingereza-pic-by-f-macha Balozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS) Jumamosi iliyopita. Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose. 8-bango-la-bts-pic-by-f-macha-2016 Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania” Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza wakazi hapa.
Wajumbe wa BTS wanaipenda Tanzania na kusimamia miradi tele kwa kujitolea bila hata senti moja. Mwaka 2015-2016 BTS imeendeleza mipango 46 ya maendeleo haya. Mama Balozi alizungumza kifupi akisisitiza masuala muhimu ya maendeleo ya elimu, uongozi mpya wa Rais John Magufuli unaosisitiza “Hapa Kazi Tu” katika kipindi cha mwaka mzima. Baada ya hapo alitumia muda mwingi kujibu maswali ya wajumbe. Aidha masuala yalijibiwa au kupewa ahadi ya kufuatiliwa kivitendo. 2-petronilla-mwakaluma-akiuliza-swali-pic-by-f-macha-2016 Mtanzania na mwanachama wa BTS, Bi. Petronilla Mwakaluma akiuliza swali 3-balozi-migiro-akijadiliana-na-wataalamu-hapa-dk-gideon-mlawa-pic-by-f-macha Balozi Migiro akijadiliana na baadhi ya wataalamu Watanzania waliokuja kumsikiliza. Aliye naye “maso kwa maso” ni mganga shupavu wa kisukari Dk. Gideon Mlawa. Kulia kwake ni mwanafunzi chuo kikuu Wales, Fadhili Maghiya. 4-dr-andrew-coulson-akiongoza-dimba-pic-by-macha-2016Mwenyekiti wa BTS, Dk Andrew Coulson akiongoza dimba. Dk Coulson mhadhiri chuo kikuu cha Birmingham aliwahi kufundisha Mlimani Dar es Salaam na kuandika kitabu cha uchumi wa Tanzania miaka ya 70 na 80. 5-watanzania-kashangwa-dk-hamza-mwakaluma-nk-pic-by-f-macha-2016Watanzania - Bw Yusufu Kashangwa, Mkurugenzi Kituo cha Biashara London, Mganga Dk Mohammed Hamza Hassan, Mganga Dk Gideon Mlawa, Mwanauchumi Dk Evans Mella na Bi Petronilla Mwakaluma. 6-bw-tony-johnson-akiuliza-swali-pic-by-f-macha-2016Bw. Tony Johnson wa Rotary Club akiuliza swali kuhusu maendeleo ya vijiji alivyofanya kazi zamani na anavyoendelea kuvitembela Tanzania. 7-balozi-migiro-akizungumza-na-watanzania-waliohudhuria-pic-by-f-macha-2016Mheshimiwa Balozi Migiro akizungumza na Watanzania waliohudhuria 9-waingereza-wanachama-waliofanya-kazi-tanzania-zamani-pic-by-f-machaWaingereza wanachama wa BTS waliofanya kazi Tanzania zamani 10-asha-yussuf-mwanafunzi-soas-london-na-dk-evans-mella-pic-by-f-machaMwanafunzi wa chuo kikuu cha SOAS , bi Asha Yussuf na Dk Evans Mella wa Investment Bank, Credit Suisse. 11-jonathan-pace-na-wanachama-wenzake-pic-by-f-macha-2016 Bw Jonathan Pace na wanachama wenzake wa BTS12-bw-aseri-katanga-akiuliza-swali-pic-by-f-macha-2016Mtanzania Bw Aseri Katanga anayepeleka Kompyuta kusaidia watoto vijijini Nigeria, Zambia, Gambia, Namibia na Tanzania akiuliza swali kuhusu viza zinazowakabali wanaojitolea katika shughuli hiyo.Shirika lake laitwa “Computers 4 Africa.” 13-balozi-migiro-akiongea-na-mwingereza-aliyekuwa-mwalimu-shule-ya-sekondari-minaki-pic-by-f-macha-2016Balozi Migiro akisogoa na Mwingereza aliyekuwa mwalimu wa shule ya sekondari Minaki, miaka ya 70. 14-mwanahabari-ben-taylor-na-mwanaharakati-ashura-kayupayupa-pic-by-f-macha-2016Mwanahabari Ben Taylor (gazeti la Tanzania Affairs) akiwa na mpigania haki za Albino, mwanafunzi Ashura Kayupayupa 15-ashura-kayupayupa-f-macha-fadhili-maghiya-na-asha-yussuf-selfie-f-macha-2016Watanzania - Ashura Kayupayupa, F Macha, Fadhili Maghiya na Asha Yussuf

No comments: