Friday, September 23, 2016

Muhimbili, MUHAS, EMAT Waendesha Mafunzo ya Kuokoa Maisha ya Wagonjwa wa Dharura na Ajali Leo

  Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Otilia Gowelle akizindua Mkutano Mkuu wa kwanza wa wataalamu wa tiba ya dharura Tanzania ambao unafanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umelenga kutoa mafunzo kwa vitendo kwa washiriki mbalimbali kutoka katika sekta ya afya nchini. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Juma Mfinanga,  Mkurugenzi wa ABBOT Fund nchini, Natalia Lobue, Rais wa Chama cha Madaktari na Wataalamu wa Tiba ya Dharura Tanzania (EMAT), Dk Hendry Sawe, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi na Mkuu wa Kitivo cha Tiba, MUHAS, Profesa Sylvia Kaaya.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi leo katika mkutano unaoendelea katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwasilisha mada leo kwenye mkutano huo leo.
 Washiriki wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano huo leo.
 Rais wa Chama cha Madaktari na Wataalamu wa Tiba ya Dharura Tanzania (EMAT), Dk Hendry Sawe akiwasilisha mada kwenye mkutano huo leo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mkutano huo Leo.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mkutano huo Leo.
 Katibu wa Chama Cha Madaktari Walio Katika Mafunzo ya Ubingwa wa Dharura Afrika, Dk Peter Mabula akitoa mafunzo ya kuokoa maisha ya watu kwa washiriki mbalimbali. Mafunzo hayo yalianza juzi katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi-Muhimbili (MUHAS).
 Washiriki wakimsikiliza Dk Mabula wakati akiwasilisha mada juu ya kuokoa maisha ya watu wanaopata magonjwa ya dharura na ajali juzi.
 Washiriki wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kuokoa maisha ya watu wanaopata magonjwa ya dharura na ajali. Mafunzo hayo yalifanyika juzi katika ukumbi wa MUHAS.

No comments: