Sunday, August 28, 2016

Serikali kubadili mtaala wa elimu wa darasa la tatu na la nne

Mmoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, akimuonesha mgeni rasmi wa mahafali ya tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda (wa pili kushoto) darubini na jinsi inavyofanya kazi. Wanafunzi 65 wa shule hiyo wanatarajiwa kuihtimu elimu ya msingi mwaka huu.
Mwanafunzi Bora katika somo la Sayansi katika Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Neema Richard akimuonesha mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda(kulia), jinsi ya kuhifadhi kiumbe mfu kwa kutumia ‘Formalin’.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Dkt. Jesse James.Kushoto ni Mkurugenzi Julius Rutabanja na Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo Machage Kisyeri na wa tatu kulia ni Mratibu wa Elimu Kata ya Segerea, Flora Vincent.
Wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Neema Richard na mwenzake wakimuonesha mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda, chura aliyehifhadhiwa kwa kutumia ‘Formalin’ katika maabara ya shule hiyo.
Mgeni rasmi wa mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda, akiangalia kifaa kinachotumika katika mfumo wa umeme wa kompyuta wakati akitembelea maonesha ya wahitimu wa shule hiyo.
Mkurigenzi Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Machage Kisyeri akiingiza kijiti kilichowashwa moto ndani ya ‘test tube’ kuzalisha hewa ya oksijeni ikiwa ni sehemu ya maonesho ya wahitimu wa shule hiyo wakionesha jinsi ya.Kulia ni mgeni rasmi wa mahafali ya tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda, akishuhudia.
Kikundi cha Skauti cha Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, kipiga saluti wakati wa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mahafali ya tano ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
Kikundi cha kwaya cha Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, wakiimba wimbo kwenye mahafali ya tano ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Skauti cha Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam,kikionesha umahiri katika mchezo wa Karate kwenye mahafali ya tano ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Aloyce Siyame akisoma ripoti ya shule kwa mgeni rasmi wa mahafali ya tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda(hayupo pichani).
Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Aloyce Siyame akisalimiana na mgeni rasmi wa mahafali ya tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda, kabla ya kumkabidhi ripoti ya shule hiyo.
Mwanasarakasi akionesha ujuzi wake kwenye mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam.
Mkurungenzi Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Machage Kisyeri akiwasilisha Taarifa ya maendeleo ya shule hiyo kwa mgeni rasmi.
Mkurungenzi Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Machage Kisyeri, akijumuika na wanafunzi wa shule hiyo kucheza ngoma ya asili ya mkoani Mara.
Wahitimu wa darasa la saba mwaka 2016 wa wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, wakiimba wimbo wa kuaga.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda akizungumza katika hafla hiyo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Dkt. Jesse James na kulia ni Mkurugenzi Mtengaji wa shule hiyo Machage Kisyeri.
Mkurugenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Imelda Machage (kushoto) na Mkurugenzi mwenzake Julius Rutabanja, wakimkabidhi zawadi mgeni rasmi katika mahafali ya tano ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda.
Mgeni rasmi katika mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Ilala Asha Mapunda (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
Wahitimu wa darasa la saba Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings ya jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye picha ya pamoja. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.

SERIKALI inajianda kufanya mabadiliko ya mtaala wa elimu wa darasa la tatu na la nne ili kukidhi mahitaji ya elimu nchini ambayo yanabadilika kulingana na muda.

Akizungumza kwenye mahafali ya tano ya Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Ilala Asha Mapunda, alisema tayari mitaala ya darasa la kwanza na la pili imeshabadilishwa.

Mapunda aliwataka wamiliki na waendeshaji wote wa shule binafsi katika manispaa ya Ilala kuzingatia kwa ukamilifu taratibu na sheria za nchi katika uendeshaji wa shule binafsi.

“Zingatieni pia mitaala inayotolewa na Serikali.Hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko katika mtaala ya madarasa ya kwanza na pili, kutakuwa pia na mabadiliko ya mtaala katika madarasa mengine la tatu na la nne” alisema Mapunda na kuongeza kuwa: “Hivi ninavyosema kuna baadhi ya walimu wetu wa darasa la tatu na la nne wako kwenye mafunzo.Lakini nina hakika kabisa hata shule za binafsi zitapata mafunzo hayo, kwa hiyo wala msijali.”

Aliwataka wamiliki na waendeshaji wa shule binafsi wasisite kuwasiliana ofisi ya elimu ya manispaa ya Ilala pindi wanapotaka ufafanuzi au maelekezo kutoka serikalini yanahitajika na Serikali itakuwa tayari kutoa msaada wowote utakaohitajika.

Alisema Serikali kwa ujumla na Manispaa yake inatambua mchango wa shule za binafsi katika kuendeleza elimu na inasisitiza na kutia moyo uwekezaji wa sekta binafsi katika nyanja ya elimu, kwani imedhihirika kwamba shule binafsi zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.

“Serikali kwa upande wake itaendelea kusaidia jitihada hizi kwa sera na miongozi ambayo imetolewa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya elimu” alisema Mapunda na kuongeza kuwa:

Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo Machage Kisyeri alisema mafanikio ya shule hiyo yametokana na filosofia yao ya kuamini katika kujenga uwezo wa mtoto kimaadili, kinidhamu na umahiri wa kitaaluma.

“Genius pia tunaamini kuwa kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa yote, hivyo shule yetu imeweka utaratibu mzuri unaowapa watoto wote wa dini tofauti fursa ya kufanya ibada pamoja na viongozi wa dini ambao tunafanya kazi nao kwa karibu sana” alisema Kisyeri.

Naye Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siyame alisema katika mahafali hayo wanafunzi 65 wanatarajiwa kuhitimu mwaka huu ambapo kati yao 23 ni wanawake na 42 ni wanaume.

Takwimu zinaonesha ufaulu wa wanafunzi wanaohitimu mitahani ya darasa la saba kutoka katika shule hiyo umekuwa ukiimarika kila mwaka ambapo mwaka 2013 wanafunzi wanne kati ya wahitimu 32 walipata daraja A na mwaka 2015 wanafunzi 40 kati ya walihitimu 57 walipata daraja A.

Aidha udahili wa wanafunzi wa shule hiyo umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2013 wanafunzi 32 walihitimu na mwaka jana wanafunzi 57 walihitimi huku kukiwa na mwanafunzi mmoja tu aliyefaulu kwa wastani wa daraja C.

Akizungumzia nafasi ya shule hiyo katika shule bora kwenye mitihani ya kitaifa, Mkurugenzi Kisyeri alisema shule hiyo ilishika nafasi ya saba katika mithani ya mwaka 2013 hadi nafasi ya tano katika mitihani ya mwaka jana katika manispaa ya Ilala.

Akizungumzia umuhimu wa michezo, Mkuu wa shule Siyame alisema Watanzania wengi hawana mwamko wa michezo, huku wazazi na wadau wa elimu bado wakiiona michezo kama chanzo cha mmomonyoko wa maadili na kupunguza morali ya kusoma shuleni.

“Kwa upande wangu ninaona wakati umefika kwa Watanzania kubadilika kifikra kwani michezo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine, pia inasemekana sasa hivi michezo ni ajira yenye malipo makubwa sana kwa hiyo tuwape fursa na tuwawezeshe watoto wetu kushiriki katika michezo.

Shule ya Genius Kings ilianzishwa mwaka 2008 ambapo baadhi ya wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kumaliza elimu msingi hupatiwa udhamini wa masomo yao ambapo kwa mwaka huu ni wanafunzi watato watasomeshwa hadi kidato cha nne.

No comments: