Sunday, June 19, 2016

Tumieni nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima kukabiliana na njaa - Waziri Mhagama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly kukagua shamba la mihogo la mkulima wa kijiji cha Nga’mbi wilayani humo Bahati Mtonyi (kushoto), aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa, Bahati Mtonyi, aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa (kulia kwake) Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje, (kushoto) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly na Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Brig.Jen, Mbazi Msuya, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje kukagua mashamba ya muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, jinsi gereza hilo lilivyo panda mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo wilayani Mpwapwa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akifurahia mihogo iliyovunwa katika mashamba ya wakulima kijijini Mazae wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, mara baada ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akinawishwa mikono na Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, mara baada ya kuonja chakula cha wafungwa wa gereza hilo, wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Katikati) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akishiriki kuonja chakula cha wafungwa wa Gereza la Mpwapwa wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Kulia kwake), Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje na (kushoto) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MUU).

WAZIRI wa ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge vijana ajira kazi na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama, amemwagiza mkuu wa wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha anatumia nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima ili kukabiliana na tatizo la njaa ambalo limekuwa likiukabili mkoa wa Dodoma.

Mhagama aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa zao la mhogo ambao walihamasishwa kulima zao hilo linalostahimili ukame ili kukabiliana na njaa.

Alisema kuwa katika kuhakikisha tatizo la njaa linakwisha mkuu wa wilaya huyo anatakiwa kuweka mikakati mipya ambayo itakuwa na tija katika kuhakisha njaa inakwisha wilayani hapo.

Aidha alisema kuwa uongozi wa wilaya hiyo unatakiwa kubuni mikakati mipya tofauti na ile ya zamani ili kutumia nguvu kazi iliyopo katika kushiriki kilimo na kusaidia kuondokana na tatizo la njaa.

“Kama mtaendelea na mikakati yenu ya kila siku tatizo la njaa halitakwisha mnatakiwa hivi sasa kutumia nguvu lazimisheni wananchi walime mazao yanayostahimilimi ukame kama mihogo na mtama”alisema Mhagama.

Alisema kuwa ofisi ya waziri mkuu kupitia kitengo cha maafa ilitoa sh. Milioni 35 kwajili ya kununua mbegu za mihogo na mtama kwajili ya wananchi ya wilaya hiyo waliokuwa wanakabiliwa na baa la njaa.

Aliongeza kuwa kwa namna alivyo jionea maendeleo ya baadhi ya wakulima waliolima mihogo wameweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na baa la njaa kwa kipindi kirefu.

“Kwa hali hii basi sisi kama ofisi wa waziri mkuu hatuna haja ya kuendelea kuleta chakula cha msaada tena huku kwakuwa zao la mihogo ambalo sisi tulileta mbegu imeweza kuwasaidia wakulima kuondokana na njaa lakini pia wengine wamejenga nyumba na kuezeka kwa bati”alisema Mhagama.

Aidha Mhagama alisema kuwa kutokana na wakulima hao kuonyesha mafanikio uongozi wa wilaya hiyo uongeze bidii katika kuhamasisha kilimo cha zao hilo.

“Inabidi muwe na hata sheria ambazo zitawalazimisha wananchi kila mmoja wao kulima heka mbili za muhogo na mbili zingine za mtama na katika hili msimbembeleze mtu tumieni nguvu ili kuweza kuondokana na na tatizo la njaa mkoani hapa”alisema.

Hatahivyo alimwagiza ofisa kilimo wa wilaya Yustina Munishi , kuhakisha idadi ya wakulima inaongezeka tofauti na iliyopo hivi sasa.

“Hadi mwakani tarehe kama ya leo nataka kuja kukaguma mashamba zaidi ya 300 na kama sitayakuta kwa idadi hiyo utakuwa huna kazi afisa kilimo”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly alisema kuwa watakipanga kuhamasisha kilimo cha zao hilo la muhogo ambalo limeonekana kuwa mkombozi wa njaa.

“Katika kipindi kijacho cha kilimo kupitia mikakati yetu tutahakikisha kila kaya inalima heka mbili za mhogo na heka mbili za mtama ili kuondokana na baa la njaa ambalo limekuwa likiikabili wilaya hiyo kila mwaka”alisema Utaly.

Naye mmoja wakulima hao Bahati Mtonyi,alisema kuwa kupitia zao hilo la muhogo ameweza kujenga nyumba na kujilipia ada kila mwaka kiasi cha sh. 600.000.

No comments: