Friday, June 24, 2016

EFM REDIO MTAANI KWAKO, LIVE LEO MWEMBE YANGA - TANDIKA.

KATIKA  harakati za kuhabarisha jamii  kwa maranyingine EFM redio imeleta mapinduzi kwa kufanya vipindi vyote  moja kwa moja kutoka mtaani kwako  leo, kuanzia kipindi cha Joto la asubuhi kinachorushwa kuanzia saa 12:00 - hadi Saa 3:00 asubuhi, pamoja na  vipindi vyote kama sports .

Headquarters, Uhondo, Ladha 3600, na kumalizia  na kipindi cha Ubaonikwa kushirikisha wakazi wa mtaa husika pamoja na kujadili mambo kadha wa kadha kuhusiana na kero, changamoto, kwa lengo la kuwaleta karibu wasikilizaji wake.
Mbali na vipindi hivyo pia kuna burudani kutoka kwa wasanii wa singeli kama M-cizo, Young Yuda, Majid Migoma, Easy Man, pamoja na Sholo Mwamba.
 Wakazi wa wilaya ya Temeke wakisikiliza matangazo ya moja kwa moja  katika viwanja hivyo vya mwembeyanga-Tandika.
 Matangazo yalianza moja kwa moja katika kipindi cha joto la asubuhi kushoto ni Gerald Hando, Adela Tillya pamoja na Paul James (PJ).
 Msanii wa singeli  M- cizo  akiwaburudisha wasikilizaji pamoja na watangazaji katika kipindi cha Joto la Asubuhi.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Diwani Isaya Charles Mwita akitolea ufafanuzi changamoto zinazoikabili manispaa ya Temeke.
  Watangazaji wa kipindi cha Sports Headquarters Kutoka kushoto ni Ibrahim Masoud (Maestro), Maulid Kitenge , Omari Katanga, wengine ni Musa Mwakisu, Yusuphu Mkule pamoja na Osca Oscar.
Wasikilizaji waliohudhuria katika eneo hilo wakijadili jambo na mmoja wa watangazaji wa Sport Headquarters Ibrahim Masoud (Maestro).

No comments: