Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze Hussein Mramba akizungumza na wafanyabiashara mbali mbali wa kitongoji cha Pera Chalinze katika mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kujadili namna ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa kipindu pindu.
KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu wafanyabiashara mbali mbali katika kitongoji cha Pera halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani wameungana na kuanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutokomeza taka zote zinakuwa zikitupwa ovyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao kilichoandaliwa kwa ajili ya kuweza kujadili mambo mbali mbali kuhusiana na suala la usafi pamoja na kupanga mikakati ya kuweza kuhakikisha wanapambana vilivyo na mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu.
Wafanyabishara hao akiwemo Rashid Kirumbi,William Mshauri Pamoja na Mwanaidi Tambiligogo walisema kwamba kwa sasa wanafanya kazi zao katika wakati mgumu sana kutokana na kitongoji hicho cha pera hakina eneo la kutupia taka hivyo kusababisha kuzagaa kwa uchafu mwingi ambao unaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi wa eneo hilo.
Aidha walisema kwamba kwa sasa katika eneo hilo la pera hakuna eneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka ukizingatia na wafanyabiashara hao wanazalisha taka nyingi kwa siku hivyo hivyo kuwapa wakati mgumu pindi wanapotaka kutupa taka.
“Hapa kitu kikubwa kikao hiki kimeandaliwa kwa lengo a kuweka mikakati ya kupambana na mlipuko wa magonjwa hususan ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa sasa umeongia katika eneo hili kwa hiyo sisis kama wafanyabiashara inatubidi tuhakikishe kwamba tunafanya usafi katika maeneo yetu ambayo tunafanyia biashara na hili suala inabidi wote kwa pamoja tushirikiane na serikai yetu,”walisema wafanyabiashara hao.
Pia walibainisha kuwa kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanatafuta eneo maalumu la kutupia taka hizo, pamoja na kuwa na gari ambalo litakuwa likipita katika maeneo mabali mbali kwa ajili ya kuweza kuzikusanya taka hizo la kwenda kuzipeleka dampo.
Nao wajumbe wa serikali ya kitongoji hicho cha pera akiwemo Simon Mbena pamoja na Nadhil Abdallah walisema kwamba kwa sasa hali ya ugonjwa wa kipindu pindu katika eneo hilo ni mbaya hivyo kunahitajika juhudi za makusudi katika kufanya usafi katika sehemu za biashara na majumbani ikiwemo sambamba na kutenga eneo kwa ajili ya dampo maalumu la kutupitia taka hizo.
Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze Hussein Mramba amekiri kutokuwepo kwa eneo la serikali lililotengwa katika kitongoji hicho kwa ajili ya matumizi ya kutupa taka,na kubainisha kwamba tayari kuna wagonjwa watano wa kipindu pindu ambao tayari wamesharipotiwa hivi karibuni katika eneo la Chalinze.
Mramba alisema kwamba nia ya serikali ni kuweza kuhakikisha kwamba wanapambana na ugonjwa huo wa kipindu pindu hivyo atashirikiana bega kwa began a wananchi wa kitongoji hicho cha pera ili kuweza kulitafutia ufumbuzi suala hilo na kuongeza kuwa kwa sasa wapo katika hatua za awali za kutafuta eneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka.
KITONGOJI hicho cha Pera kilichopo katika mamlaka ya mji mdogo Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani hakina dampo la kutupia taka, na kupelekea wafanyabiashara na wananchi kuamua kuzitupa sehemu yoyote hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuzagaa kwa uchafu huo ambao umedai unasababisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki cha masika.
No comments:
Post a Comment