Tuesday, April 5, 2016

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Bw. Ibrahim Mussa (kulia) akiongea na Kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Arusha Bi. Maria Kirombo (kati) na Mhifadhi wa Idara ya Ulinzi Bw. Haima Hera muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa ziara fupi hifadhini hapo. 
Kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Arusha Bi. Maria Kirombo akitoa maelezo mafupi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kabla ya kuanza kwa ziara fupi katika Hifadhi ya Arusha. 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ndani ya basi dogo wakiangalia wanyama aina ya nyati wanaopatikana katika Hifadhi ya Arusha. 
Twiga watatu wakionesha mbwembwe zao mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii. 
Waheshimiwa Joseph Kasheku ‘Msukuma’ (kulia) na Shaban Shekilindi (Lushoto) wakiwa na fuvu la mnyama nyati walilolikuta hifadhini hapo na kupiga nalo picha na kisha kuliacha hapo hapo. 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika picha ya pamoja mbele ya Ziwa Momela katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani (kushoto),Mhe. Joseph Kasheku ‘Msukuma’, Mhe. Kemilembe Julius na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa katika picha ya pamoja. 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipowasili Hifadhi ya Taifa ya Arusha. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

No comments: