Friday, March 4, 2016

SIMU TV:HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Uchaguzi wa Meya jiji la Dar es salaam waendelea kuwa gumzo na kupelekea viongozi wa Chadema kuvamia ofisi za mkurugenzi wa jiji.https://youtu.be/F3dFAyF1zcc
  
Mkuu wa mkoa wa Morogoro akipongeza chuo kikuu cha Mzumbe kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuchangia na kuboresha elimu nchini baada ya kutoa msaada wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Mindu.https://youtu.be/vQlF4LVok2U

 Jeshi la ulinzi la wananchi watanzania JWTZ lawaaga rasmi makamanda 16 waliomaliza mda wao wa utumishi katika jeshi hilo kwa gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yao.https://youtu.be/gXVeLsNLOL4
  
Halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha yawasimamisha kazi watumishi 3 wa idara ya ardhi kwa tuhuma za upotevu wa fedha za viwanja na uuzaji wa viwanja bila kufuata taratibu na kuisababishi serikali hasara. https://youtu.be/azV9-1HkL5s  
  
Naibu waziri TAMISEMI Suleiman Jaffo afanya ziara kwenye soko la Ilala Boma na kupokea kero lukuki kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya kazi zao katika soko hilo. https://youtu.be/PoVlqSs-Txs 
  
Watumishi wa idara ya ustawi ya jamii waaswa kuacha tabia ya kukaa ofisini na badala yake watembelee maeneo mbalimbali ili kuweza kubaini changamoto zinazoikabili jamii hususani watu wenye ulemavu. https://youtu.be/3MCmKmkmd_k  
  
Tume ya ushindani nchini kwa kushirikiana na polisi yaendesha operesheni maalum ya kukamata simu feki za Samsung katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo. https://youtu.be/F9oRW-ov_Qc  
  
Wabunge mkoa wa Tabora waishauri serikali kumnyanganya mwekezaji wa kiwanda cha nyuzi mkoani humo kwa tuhuma za kushindwa kukiendeleza na kuwanyima wananchi fursa za ajira.https://youtu.be/Sgqc06h1fHY
  
Waziri wa maliasili na utalii Prof. Jummane Maghembe awasimamisha kazi watumishi 5 wa mamlaka ya hifadhi ya Ngororo kwa ubadhilifu wa fedha za umma; https://youtu.be/J4q2FAoTpNg  

Serikali mkoani Kagera yaitaka kampuni ya ujenzi ya Chicco kuwapatia mikataba ya ajira wafanyakazi wake;https://youtu.be/qHLHq5H19c4  
  
Baadhi ya wananchi wa Itilima mkoani Simiyu waiomba serikali kukamilisha haraka ujenzi wa mradi wa maji safi ili waupekane na shida ya maji; https://youtu.be/rPRNoN4X95g  
  
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Uguzi wilayani Chamwino mkoani Dodoma wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati;https://youtu.be/BNyMHsBe5Qg  
  
Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ lawaaga majenerali kumi na sita waliomaliza muda wao wa kulitumikia jeshi hilo;https://youtu.be/h5KsOpVK8Dc
  
Serikali yazindua mpango wa urasimishaji wa makazi kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo bado hayajapimwa;https://youtu.be/Jcwvgy4gEV0  
  
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa aitaka mamlaka ya bandari mkoani Tanga kutumia njia ya kieletroniki ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato;https://youtu.be/ERmCfJ3dgr0   
  
Shirika la umeme Zanzibar linatarajia kuingia mikataba na makampuni ya simu visiwani humo ili kurahisha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wateja wake;https://youtu.be/BAP18dtK1Do  
  
Inaelezwa kuwa mfumuko wa bei visiwani Zanzibar waongezeka kwa zaidi ya  asilimia moja kutokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa ya vyakula; https://youtu.be/4JRQ4dxGTRk  
  
Shirikisho la soka  nchini TFF latoa ratiba ya michezo ya robo fainali ya kombe la shirikisho inayotarajia kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu; https://youtu.be/dT895zUNrJ0  
  
Timu ya taifa ya soka ya wanawake Twiga Stars yaambulia kipigo cha goli 2-1 dhidi ya ya timu ya taifa ya Zimbabwe katika mchezo wa awali wa kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika kwa wanawake; https://youtu.be/Wq_7WuUcCwc

No comments: