Monday, March 14, 2016

MRATIBU WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA HAPA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo ambaye pia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akimweleza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nia ya Mashirika hayo ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika masuala mbalimbali. Bw. Rodrequez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake leo. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga akimwelezea  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez (katikati) mipango ya Wizara yake ambayo inaweza kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. Bwana Rodriguez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake leo kuelezea nia ya Mashirika hayo ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo ambaye pia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga mojawapo ya makabrasha ya Mashirika hayo yenye mipango ya maendeleo ya kuisaidia Tanzania. Bw. Rodriguez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake kuelezea nia ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kutekeleza baadhi ya majukumu yake. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga akisisitiza jambo kuhusiana nia ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kuisaidia Wizara yake. Katikati ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez aliyemtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake leo kuelezea nia ya Mashirika hayo ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga akimshukuru Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko hapa nchini Bw. Alvaro Rodrigues kwa kueleza nia ya Mashirika hayo kutaka kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Bw. Rodrequez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake leo. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI– WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).

No comments: