Wednesday, March 9, 2016

Dkt. Mwanjelwa awafuta machozi wanafunzi waliounguliwa bweni Iyunga Mbeya


Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akimkabidhi mashuka 40 na magodoro 20, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi (wa pili kutoka kushoto), kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao. 
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA
Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akizungumza jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga ya Jijini Mbeya, alipoenda kukabidhi msaada wa mashuka 40 na magodoro 20, kwa niaba ya Mbunge Dkt. Mwanjelwa leo, kufuatia wanafunzi hao kuunguliwa na bweni moja juzi.
Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akimkabidhi mashuka 40 na magodoro 20, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi (wa pili kutoka kushoto), kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical ya Jijini Mbeya, wakibeba magodoro 20 na mashuka 40, kwenda kuyahifadhi baada ya kukabidhiwa na mwakilishi wa Mbunge wa viti maalim mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa leo.
Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akimkabidhi mashuka 40 na magodoro 20, mkuu wa shule ya Iyunga Technical ya Jijini Mbeya, Edward Mwantimwa, kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi (katikati), akimshukuru Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya, (hayupo pichani) Dkt. Mary Mwanjelwa, kwa msaada wake alioutoa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.
Kulia ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akiwakabidhi mashuka 40 na magodoro 20, wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.


Na, Gordon Kalulunga, Mbeya


MWENYEKITI wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mary Mwanjelwa, ambaye ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya (CCM), amewapa pole wanafunzi wa shule ya ufundi Iyunga Technical School, kufuatia kuungua kwa bweni la shule hiyo juzi, iliyopo Jijini Mbeya.

Akizungumza kwa niaba yake shuleni hapo leo, msaidizi wa Mbunge huyo, Tumaini Ambakisye Mwakatika, alisema Dkt. Mwanjelwa ameguswa na kusikitishwa na tukio hilo na kwamba ameamua kutoa msaada wa magodoro na mashuka kwa wanafunzi walioathirika.

“Mhe. Dkt. Mwanjelwa kama kiongozi mwanamke, amesikitishwa na tukio la moto katika bweni la wanafunzi lililotokea siku ya Jumatatu na ametumia siku ya maazimisho ya wanawake kuja kuwaona kwa kutoa magodoro 20 na mashuka 40 na akitoka Dar es Salaam ameahidi kufika hapa shuleni kwa ajili ya kuja kuwaona” alisema Tumaini.

Akizungumza kwa njia ya simu na www.kalulunga.blogspot.com Dkt. Mwanjelwa alisema maandiko matakatifu yanasema kuwa lieni na wanaolia, hivyo licha ya kuwa mbali, ameona atangulize msaada huo.“Mimi ni mama, nimeumizwa sana na tukio hili la kuungua bweni la shule ya Iyunga ambayo ni moja ya shule za kihistoria katika mkoa wetu wa Mbeya, nashukuru Mungu nimepokea taarifa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mbeya  ndugu Nyerembe Sabi Mnasa, kuwa hakuna mwanafunzi ambaye ameathirika na moto huo” alisema mbunge huyo.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Sabi Mnasa, alimwambia msaidizi wa mbunge huyo kuwa, msaada huo ni mkubwa na Dkt. Mwanjelwa anapaswa kupewa sifa katika kujitoa kwake hasa kwa wahitaji na tayari tume imeundwa kuchunguza tukio hilo ambalo lina sentensi za utete ikiwemo kuwa wiki moja lilipoungua bweni la kwanza hakukuwa na umeme shuleni hapo.

Akipokea msaada wa magodoro 20 na mashuka 40 yaliyotolewa na Dkt. Mary Mwanjelwa shuleni hapo, mkuu wa shule hiyo, Edward Mwantimwa, huku akionekana ni mtu ambaye hayupo kwenye hali yake ya kawaida, alishukuru na kwamba kwa sasa wapo katika kipindi kigumu sana.

“Namshukuru sana mbunge Mwanjelwa kwa moyo huu wa utoaji na kwa kuwaza kwa ajili yetu” alisema Mwalimu Mwantimwa.Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Dkt. Stephen Mwakajumilo ameumbia mtandao huo wa kalulunga blog kuwa “Sisi kama bodi ni kupokea msaada wa aina yeyote kote duniani, tunawashukuru waliojitokeza kutoka CCM na Chadema. Tunaomba Dkt. Mwanjelwa atusaidie kuwashawishi wengine na viongozi tutafakari pamoja kuhusu shule zote za zamani nchini hasa miundombinu ya shule hizo. Alisema.

No comments: