Thursday, April 30, 2015

STOP FLOCKING IN SOUTH AFRICA, PRESIDENT MUGABE

Heads of State and government of the Southern African Development Community (SADC), meeting in Harare, Zimbabwe yesterday condemned the recent attacks against African migrants in parts of Durban and Johannesburg in South Africa. The summit meeting was reacting to a briefing by South Africa President Jacob Zuma on the nature of the xenophobic attacks and measures taken by his government to restore peace.

According to a communique issued after the meeting, "Summit commended the measures that the government of South Africa has put in place and resolved to work together to deal with the situation and ensure it does not recur." The attacks affected the citizens of SADC member countries of Zimbabwe, Mozambique, Malawi, Zambia and Tanzania, which were forced to evacuate their people.

The violence heightened tension between South Africa and its neighbours, some of whom threatened retaliatory measures. But briefing the media after the summit yesterday, The SADC Chairman, President Robert Mugabe, said the situation should not be blamed on South Africa alone. He said an virtually unchecked influx of migrants from neighbouring countries was stretching resources to the limit in South Africa, where the majority blacks were living in dire conditions.

"Only the whites are living well there. Our people should not have the instinct to rush to Johannesburg in the false hope that it is heaven," he said. The SADC Chair said one way to arrest the influx was for SADC member countries to improve their economies and attract their youth to stay and work at home. Hundreds of Zimbabweans, Malawians, Mozambicans and Zambians were evacuated following the attacks, but millions more, who are largely unskilled, remain in South Africa.

Twenty six Tanzanians were facilitated by the government to return home last week and the Tanzania High Commission in Pretoria is looking for others who may wish to return home. There was no Tanzanian among eight foreigners reported to have been killed in the attacks.

President Zuma has been quoted in the media as saying he would address the root causes of the xenophobic attacks, which he said were poverty, unemployment and immigration. An estimated 53 percent of the South African population lives below the poverty line, according to the United Nations. (Ends) .


Arrival of Dr. Bilal in Zimbabwe .
Vice President of the United Republic of Tanzania, H.E Dr. Mohamed Gharib Bilal is received by Tanzania Government Officials when he arrived at the Melkles Hotel in Zimbabwe. Dr. Bilal represented President Jakaya Mrisho Kikwete at the SADC Heads of State Extra Ordinary Summit on Industrialization held in Harare yesterday.

High Commissioner of Tanzania to Zimbabwe, H.E Adadi Rajab makes a briefing to the Vice President prior the SADC Summit. On the left is the Minister of Industry and Trade, Hon. Dr. Abdallah Kigoda (MP).
High Commissioner of Tanzania to South Africa, H.E Radhia Msuya contributes a point during a briefing session towards SADC Summit.

IFIKAPO MACHI MWAKANI TATIZO LA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM LITAKUWA HISTORIA

 Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
IFIKAPO machi mwakani tatizo la umeme jijini Dar es Salaam itakuwa historia  kutokana na kukamilika  kwa miundombinu  ya mitambo ya  umeme ifikapo machi mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene katika ziara ya  ukaguzi wa miradi ya umeme ya  Kurasini, Mbagala pamoja na Kinyerezi  jijini Dar es Salaam leo.

Ziara hiyo  iliyoanzia katika mitambo ya Umeme Wizarani hapo na kuelekea,Kurasini na Mbagala ikiwa na lengo la  kusogeza miundombinu ya umeme karibu na watumiaji wa umeme.

Simbachawene amesema kuwa  kuna miradi minne ambayo mpaka sasa inafanyiwa kazi kwa uhakika  inayotegemewa kusambaza Umeme kwa watumiaji bila kuwa n amatatizo ya  umeme.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  amesema kuwa matatizo mbalimbali ya  ununuzi wa Luku za umeme nayo yanafanyiwa kazi kwa  kuyahimiza makampuni nayoshirikiana na TANESCO katika uuzaji wa umeme ili waweze kuimarisha huduma hizo.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  kuhusiana na uboreshaji wa  Mtambo wa umeme uliopo katika wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene  akikagua Mtambo wa umeme uliopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Mitammbo ya umeme iliyopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akizungumza na wandishi wa habari katika  Ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa miradi ya umeme jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo na  Manirabona Emmanuel meneja wa Project wa TANESCO kuhusiana na uboreshaji wa mitambo ya Umeme ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa project wa Tanesco Manirabona Emmanuel akimwonyesha Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene  jinsi mitambo ya Umeme itakavyo jengwa katika Mitambo ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Mitambo ya umeme ya Mbagala jijini Dar es Salaam. Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Mradi wa kutekeleza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini wawanufaisha wakulima

Afisa kilimo wa mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) Nicholas Johanes (wa kwanza kulia aliyechuchumaa aliyeshika simu) akitoa maelezo kwa kulima(nyuma yake) kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa siku ya wakulima iliyofanyika katika kijiji cha Laela wilaya ya Sumbawanga . Wapili kushoto ni Joseph Mwangono , Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga.
Wakulima wakiangalia moja ya shamba darasa Mbeya vijini . Aliyechuchumaa ni Nicholas Johaness, afisa kilimo (ACTN)

Na mwandishi wetu 
Mradi wa  kutekeleza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini umekuwa na mafanikio kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao  kwa kutumia kilimo hifadhi lakini changamoto kubwa imeonekana ni ukosefu wa masoko .

Mradi huo ambao unafadhiliwa na mtandao wa mapinduzi ya kijani barani Afrika  (AGRA )unatekelezwa na mashirika manne katika wilaya sita za mikoa ya Mbeya na Rukwa katika mazao manne kutokana na eneo husika ambayo ni Mahindi , mpunga , Soya na maharage  kwa kutumia kilimo hifadhi .

Katika siku ya wakulima iliyofanyika kijiji cha  Laela wilaya ya  Sumbawanga , Mwenyekiti wa chama cha ushiliki mazao na masoko Laela Amcos Limited  bwana Edom Mwaisemba amesema wakulima wamelima kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kuzalisha mazao mengi lakini kinachowakwamisha ni soko .

‘’ Kwa mfano  mwaka jana tulipata tani 2,500 lakini tukashindwa wapi tutapata soko . Tunauomba mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) kwasababu umetufundisha jinsi ya kulima na tumelima kikamilifu kwa kufuata kanuni bora  na tunaweza kupata hadi tani 3,500 kwa hiyo tunauomba ututafutie soko’’ alisema bwana Mwaisemba .

Bwana shamba kutoka taasisi ya kilimo , biashara tegemezi ya mazao mengi ya mkoani Ruvuma(RUCODIA)  bwana Evaresto Joshua amesema kwa kuondoa changamoto ya soko wamekubaliana na mashirika mengine ya mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika  (ACTN) , CNV na micro finance limited kuwatumia mawakala wa pembejeo pia kununua mazao .

Changamoto ya matumizi bora ya mbegu pia imejitokeza katika siku hiyo ya wakulima ambapo wakala wa mbegu SEEDCO Tanzania Limited imewashauri wakulima kutotumia mbegu kutoka nje  ambazo hazijapimwa  na taasisi za ndani ya nchi .

‘’ Tunajaribu kuwasisitiza wakulima kuhusu matumizi bora ya mbegu bora . Lakini zaidi tunasisitiza uagizaji na ununuzi wa mbegu ambazo zinatoka nchi za jirani ziwe zimepimwa na taasisi mbali mbali za nchini mwetu ‘’ alisema bwana Joshua Zuberi , afisa mauzo  kutoka wakala wa mbegu  SEEDCO Tanzania Limited .

Nao wakulima wamesema kilimo hifadhi kimewasidia kuhifadhi udongo na pia  kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji  ikilinganishwa na awali .

 ‘’ Unakuta mwanzoni heka moja ulikuwa unatumia shilingi 500,000 lakini kwa sasa hivi angalau inapungua hadi shilingi laki mbili . Unaposema kupunguza gharama ni sehemu zote kuanzia uandaaji wa shamba . Kwa mfano kuandaa shamba kunahitaji kutumia moto lakini sasa hivi tunahifadhi udongo tunafukia mlemle ndani ‘’ alisema bwana Ezebius Chapita , mkulima kijiji cha Lula .

 ‘’ Faida nyingine za mradi huu ni kusogeza huduma ya ugani  karibu kwa namna ya kwamba sio kila kijiji kina afisa ugani lakini kutokana na mafunzo haya ya kilimo hifadhi tumeweza kuwasaidia wakulima viongozi kutoa taarifa za ugani kwa wakulima wetu na pale inaposhindikana wanaweza kuwasiliana na sisi kwa kuwasaidia zaidi .’’ alisema Nicholas Johanes  , afisa kilimo wa mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika  ( ACTN)

Naye Joseph Mwangono , afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga ambaye alimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Sumbawanga katika sherehe hizo alisema kumekuwa na mafanikio kutokana na wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo 
‘’ Kwa upande wa zao la mahindi wengi sasa wanapanda kwa kutumia mistari ,wanatumia mbolea na wanapalilia kwa wakati tatizo tu linakuwa soko la zao hilo la mahindi . Kwa zao la maharage zamani walikuwa wanapanda kwa kumwagilia lakini sasa hivi wanapanda kwa mistari na kutumia mbolea ‘’ alisema bwana Mwangono . 

Kanuni za kufuata katika kutumia kilimo hifadhi ni pamoja na kufunika udongo kwa kutumia mazao funika au mabaki ya mazao , kutosumbua udongo na kupanda bila kulima kwa kutumia zana maalum .
Kwa mujibu wa ACTN , mafanikio ya kwanza katika maeneo maalum Tanzania ni pamoja kupunguza mmonyoko wa udongo kwa zaidi ya asilimia thelathini .

Serikali yadhamiria kukamilisha Miradi ya Kitaifa ya Kimkakati

Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Sehemu ya Wabunge waliohudhuria uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima wakimsikiliza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16.
viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 uliokuwa ukifanywa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima. Picha na Saidi Mkabakuli.
Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.

Na Saidi Mkabakuli
Serikali imesema kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miradi ya kitaifa ya kimkakati iliyoibuliwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo unaofikia kikomo mwaka ujao wa fedha wa serikali.
Hayo yalisemwa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Nagu alisema kuwa mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu, serikali imefanikiwa kutandika reli za uzito wa ratili 56.12 kwa yadi kwa umbali wa km 9 kati ya stesheni za Lumbe, Mto Ugalla na Katumba; kukamilisha malipo ya ununuzi wa mabehewa 274 ya mizigo ambapo mabehewa yameshaanza kupokelewa Novemba 2014; kukamilika kwa matengenezo ya njia ya reli iliyoharibiwa na mafuriko katika maeneo ya Ruvu – njia panda ya Mruazi.
Waziri Nagu aliongeza kuwa kwa upande wa Barabara hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa kilometa 502.6 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kilomita 560, na ukarabati wa kilomita 78.8 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kukarabati kilomita 131.5. Kwa upande wa madaraja hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa madaraja ambapo daraja la Kigamboni limefikia asilimia 75, Sibiti asilimia 22, Kilombero asilimia 26, Mbutu asilimia 99, Lukuledi II asilimia 25 na Kavuu asilimia 36.
Katika sekta ya Uchukuzi, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa shehena iliyohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam kufikia tani milioni 14.3 Machi 2015 dhidi ya lengo la tani milioni 13.0 kwa mwaka 2014/15; kuongezeka kwa ufanisi wa bandari katika kupakua magari kwa kila shifti moja ya saa 8 kufikia magari 886 kwa shifti kufikia Machi 2015 ikilinganishwa na lengo la magari 600 kwa shifti katika mwaka 2014/15; kupungua kwa muda wa meli kupakia na kupakua mizigo bandarini kutoka lengo la wastani wa siku 5 mwaka 2013/14 hadi wastani wa siku 3.7 kufikia Machi 2015; kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa malipo kwa njia ya mtandao mwezi Julai, 2014; na kuanza  kutoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam kwa masaa 24 kwa siku zote za juma. Aidha, kwa upande wa bandari ya Bagamoyo, hatua iliyofikiwa ni kusainiwa kwa makubaliano ya ujenzi wa bandari; na kutangazwa kwa zabuni kwa ajili ya kupata wawekezaji katika bandari za Mtwara na Mwambani -Tanga.
“Katika sekta ya nishati, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542) Machi 2015, na ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi Madimba (Mtwara) na Songosongo (Lindi) umefikia asilimia 86.9 ambapo unatarajiwa kukamilika Juni 2015. Kwa upande wa usambazaji wa umeme vijijini, wateja wapya 2,602 wameunganishiwa umeme katika mikoa ya Simiyu, Singida, Kagera, Tanga, Ruvuma, na Iringa,” alisema Dkt. Nagu.
Kwa mujibu wa Waziri Nagu, shughuli nyingine zilizotekelezwa nia katika sekta ya nishati, ni pamoja na kukamilika kwa usimikaji wa mitambo 4 ya kufua umeme yenye uwezo wa jumla ya MW 150, kuendelea na ujenzi  wa vituo vya kupoza na njia za kusafirisha umeme, na kuendelea na ujenzi wa  karakana, majengo ya utawala, na barabara za ndani katika mradi wa Kinyerezi I; kukamilisha ulipaji fidia kwa eneo la Makambako katika mradi wa usafirishaji umeme wa Makambako - Songea;  na kuanza ujenzi wa nguzo za njia ya umeme katika mradi wa msongo wa kV 400 wa Iringa – Shinyanga.
Akiwasilisha kazi zilizotekelezwa katika sekta  ya Maji, Dkt. Nagu alisema kuwa  ulazaji wa mabomba katika mradi wa maji Ruvu Chini kutoka Bagamoyo hadi Dar es Salaam kazi ambayo imekamilika kwa kilomita 52.43 kati ya kilomita 55.93 za mradi sawa na asilimia 93.8; kwa upande wa mradi wa maji Ruvu Juu: mkandarasi amekamilisha utafiti wa udongo na uchunguzi wa awali wa mahali yatakapojengwa matanki Kibamba na Kimara; na kwa upande wa mradi wa Bwawa la Kidunda,  wananchi wamelipwa fidia ya shilingi bilioni 7 kupisha ujenzi wa barabara na eneo litakapojengwa bwawa.
“Kwa upande wa miradi ya maji vijijini, jumla ya miradi 123 ya maji ilijengwa na kukamilika. Idadi hii imenufaisha wananchi wapatao 463,750 na kuongezeka kwa ufanisi katika masuala ya ununuzi wa huduma katika mikataba kutoka siku 265 hadi siku 90. Aidha, Serikali imeendelea na ujenzi wa mabwawa ambapo bwawa la Iguluba (Iringa) na Wegero (Mara) yamekamilika. Vile vile, ujenzi wa bwawa la Kawa (Rukwa) umefikia asilimia 95, bwawa la Sasajila (Dodoma) asilimia 66.09 na Mwanjoro (Shinyanga) asilimia 45.4,” aliongeza Waziri Nagu.
Katika sekta ya kilimo, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: kupatikana kwa hati za mashamba mawili ya Bagamoyo na Mkulazi; maghala 30 yamekarabatiwa na kupatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbozi na Momba.  Vile vile, skimu 30 za umwagiliaji zimepatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbarali, Kyela na Iringa; na mafunzo juu ya kubaini na kudhibiti visumbufu, matumizi bora ya maji, utunzaji na matengenezo ya miundombinu ya umwagiliaji na kutumia mwongozo wa uendeshaji skimu za umwagiliaji yametolewa.  Aidha, ujenzi wa maghala 2 katika Wilaya ya Mlele umekamilika.
Vile vile katika sekta ya viwanda, Waziri Nagu alizitaja kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya Itoni - Mkiu - Liganga na Mchuchuma kwa kiwango cha changarawe ili kuwezesha mitambo kufika maeneo ya Mchuchuma na Liganga; na kuanza uthamini wa mali za wananchi watakaohama eneo la Mchuchuma. Vile vile, fidia shilingi bilioni 53 imelipwa katika eneo la kujenga kituo cha Biashara na Huduma Kurasini; na fidia ya shilingi bilioni 7 imelipwa katika eneo la uwekezaji Bagamoyo na Serikali imesaini mkataba na kampuni ya China Mechants Holding International kwa ajili ya kujenga bandari na eneo la viwanda. Aidha, katika kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua viluwiluwi wa mbu, Kibaha, kazi ya ufungaji wa mitambo na ujenzi wa miundombinu inaendelea na inatarajiwa kukamilika kabla ya Julai, 2015.
Akizungumzia upande wa maendeleo ya rasilimali watu, Dkt. Nagu alisema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na kuendelea kugharamia wanafunzi 159 wanaoendelea na mafunzo katika fani za mafuta na gesi kwa ngazi mbalimbali za mafunzo ndani na nje ya nchi ambapo wanafunzi 124 wanagharamiwa na Serikali na wanafunzi 35 wanagharamiwa na nchi wahisani; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vikuu na vyuo vya ualimu, ufundi na ustawi wa jamii.
Kwa upande wa utafutaji wa rasilimali fedha, Waziri Nagu alisema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania inatumia kanzidata bora inayohifadhi taarifa inayoweza kuthaminisha bidhaa na hivyo kutoa makadirio bora zaidi ya viwango vya kodi. Vilevile, alisema kuwa tozo kwa ajili ya uwekezaji katika elimu umeanza Julai 2013 ikiwa asilimia 2.5 ya mapato ghafi ya kampuni za simu.
“Katika sekta ya fedha, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuongezea Benki ya Maendeleo ya Kilimo mtaji wa shilingi bilioni 60; kuendelea kuongeza mtaji wa Benki ya Rasilimali kufikia shilingi bilioni 212 ambapo mtaji kutoka Serikalini ni shilingi bilioni 152.2 na shilingi bilioni 59.8 zimetokana na malimbikizo ya faida; na  mali za Benki ya Maendeleo ya Wanawake Tanzania ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 26.5 mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 34.8 mwaka 2014,” alisema Dk. Nagu.
Kuhusu eneo la huduma za utalii, Dkt. Nagu aliongeza kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na usanifu wa ujenzi wa Utalii House awamu ya pili na kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji mapato (utalii, uwindaji na upigaji picha). Aidha, idadi ya watalii kutoka nje iliongezeka kutoka watalii 1,090,905 mwaka 2013 hadi watalii 1,102,026 mwaka 2014. Vile vile mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.81 mwaka 2013 hadi dola za Marekani bilioni 1.98 mwaka 2014.
“Kwa upande wa Biashara, hatua iliyofikiwa ni kurekebisha sheria ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kutoa  elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu mfumo huo; kuanzishwa kwa kampuni ijulikanayo kama Tanzania Mechantile Exchange plc kusimamia na kuendesha soko la mazao ya bidhaa na kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya mipakani, Kikanda na Kimataifa,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Dkt. Nagu maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/16 yamezingatia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16). Aidha, Mpango huu umezingatia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini – MKUKUTA II (2010/11 – 2014/15), Malengo ya Milenia, Mwongozo wa Mpango na Bajeti  kwa mwaka 2014/15; Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2014/15 yaliyojadiliwa na Bunge Novemba, 2014; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2010 – 2015); na sera na mikakati ya kisekta.

WANAZUONI WAJADILI MUSTAKABALI WA TANZANIA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI

Jaji Francis Mtungi akifunguja mkutano wa wadau wa siasa  wa uimatishaji demokrasia ya vyama vingi
Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.


Dk. Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.

Dk Bana alisema hayo jana akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama vya siasa kwa ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.

Profesa Killian alitaka kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake kuhusu ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini kinastahili kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu ambapo viashiria vipo.

Dk Bana alisema kama watu hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata sheria na kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.

Alisema watu kama wanaona wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo zinaonekana ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu hizo zenye matatizo kwa kufuata utaratibu.

Katika shauri hilo la viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning) ili iweze kukabiliana navyo mapema.

Akizungumzia kama Tanzania ni nchi ya demokrasia Dk. Bana alisema kwamba kuna maendeleo makubwa yamepatikana tangu mtindo wa vyama vingi kuingia nchini miaka 23 iliyopita.

Alisema demokrasia haijengwi kwa siku moja, ina safari ndefu yenye milima na mabonde na wakati mwingine watu wasifike.
Mkurugenzi UNDP Philippe Poinsot  akizungumza katika mdahalo
Mkurugenzi wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na kiraia katika mkutano huo.

Aidha alisisitiza kwamba demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania wanastahili kujivuna kwa hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali ambayo hata mataifa mengine ya Ulaya hayajafikia.

Alisema mwaka 1994 wakati taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na vyama 13 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza kuna vyama 22 vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa umetanuka zaidi.

Pia alisema mafanikio mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuandika inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini kadhia hizo haziondoi ukweli kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari.
Dk bana akizungumza katika mdahalo
Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.

Alisema taifa hili halina sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na changamoto zake katika siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa unazidi kutanuka.

Alisema pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.

Alisema kutanuka kwa wigo wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa) kunatakiwa kwenda sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi wa utamaduni wa vyama vingi.

Alisema pia kuna haja ya kuimarishwa kwa taasisi zinazosaidia utamaduni huo kama Tume huru ya Uchaguzi, Bunge na hata mfumo wa utawala ambapo wakuu wa mikoa na wilaya wasiwe katika hali ya kikada bali wale wanaoweza kutekeleza majukumu yanayostahili katika maeneo yao.
jaji Mutungi akiwa na Mkurugenzi UNDP Poinsot
Jaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.

Aidha alisema kwamba vyama vingi vya siasa vinafanyakazi ya uanaharakati badala ya kuwa na itikadi ya kuifuata .

Alizungumzia pia haja ya vyama vya upinzani kujivunja na kuanzisha chama kimoja na kutengeneza mkakati wa kutwaa dola huku akisema muungano wa Ukawa kwa sasa una mushkeri zaidi badala ya kusaidia kujiandaa kutwaa dola.

Katika mdahalo huo ambao ulielezwa na Msajili wa vyama vya Siasa jaji Francis Mutungi, si mkusanyiko wa kufanya kampeni ya uchaguzi bali jukumu la ofisi ya msajili hasa kuelekea uchaguzi mkuu, washiriki wake pia walielezwa changamoto za siasa za vyama vingi.

Profesa Rugumamu alisema kwamba katika tafiti aliyoifanya yeye na wenzake katika nchi 15 za bara la Afrika wamekumbana na changamoto takribani saba ambazo ni kikwazo katika kupata na kukuza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
IMG_4917
Jopo la wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana, Profesa Meena, Profesa Rugumamu na mwishoni ni msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.

Miongoni mwa changamoto hizo ni vyama vikongwe na utamaduni wake kushindwa kuainisha kati ya mamlaka ya dola na vyama vyenyewe, kuwepo kwa vyama vya kikanda na kidini katika kipindi cha mpito katika demokrasia ya vyama vingi, wanasiasa kubadili katiba waendelee kutawala, vyama na wanachama kutojua haki na wajibu wao kutokana na kutofundishwa uraia tangu awali.

Pia alizungumza uadui unaojijenga kwa nchi ambazo zimetoka vitani na uanzishaji wa makundi ya ulinzi ya vyama ambavyo husababisha mitafaruku wakati wa uchaguzi au kwenye uchaguzi na matumizi ya fedha yasiyojulikana kwa ama kukosa sheria au sheria kuwapo na watu kutoizingatia.

Alisema dosari zote hizo zinatikisa ujenzi wa utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.

Awali akimkaribisha Jaji Mutungi kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot alisema Umoja wa mataifa umefurahishwa kwa wadau wa siasa nchini Tanzania kuwa na mazungumzo yenye lengo la kustawisha amani kuelekea uchaguzi na kutengeneza mfumo wa majadiliano kama kukiwepo na kutokuelewana.

Alisema mkutano huo walioufadhili ni sehemu ya makubaliano ya Ofisi ya Msajili na UNDP kupitia mradi wake wa kuimarisha demokrasia (DEP) yenye kulenga kujenga uwezo na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maelewano ndani ya vyama na kitaifa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
IMsimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian
Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.

Alisema ni matumaini yake kwamba mkutano huo utatengeneza mustakabari bora wa Tanzania kuwa na uchaguzi huru na wa amani.

Alisema kutokana na ushindani, uchaguzi unaweza kuleta matata kwa hiyo ni vyema kama wadau wataliangalia hilo na kuona namna ya kutanzua matata ili taifa libaki na amani na kusonga mbele katika maeneo yote ya jamii.

Naye Jaji Mutungi aliwaasa washiriki kutambua kwamba hakuna sababu ya kukamiana na kukomoana miongoni mwa vyama vya siasa kwani wote wanajenga nyumba moja na kimsingi hawana sababu ya kugombania fito.
Alitaka wadau kucheza mchezo wa siasa kwa maridhiano ili wasibomoe misingi ya amani ya taifa na mafanikio yake.

Alisema lengo la mkutano huo ni kuweka sawa dhana ya demokrasia ya vyama vingi na kutafuta majibu ya changamoto zinazokabili pasipo kuvunja amani ya nchi.
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.
Profesa Rugumamu akizungumza
Profesa Rugumamu akizungumza.
IMG_4861
Baadhi ya washiriki wakijadiliana.
IMG_4879
Washiriki wa mkutano wakijadiliana.
wanamdahalo wakiwa makini
Wanamdahalo wakiwa makini.

ZIMBABWE YAIPA MAJENGO SADC KWA AJILI YA KITUO CHA KUFUNDISHIA WALINDA AMANI


Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Robert Mugabe akiangalia Hati Miliki ya Majengo ambayo Serikali ya Zimbabwe imetoa kwa SADC kuwa Kituo cha Kufundishia Walinda Amani. Hati hiyo ilikabidhiwa kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax anayeonekana kushoto. Majengo hayo yapo kwenye kiwanja chenye ukubwa wa ekari 16 ambayo Zimbabwe imetoa bure kwa SADC kama mchango wake wa kuhamasisha amani na utulivu barani Afrika.
Rais Mugabe akionge machache mara baada ya kukabidhi Hati Miliki ya majengo ya Kituo cha Kufundishia Walinda Amani.

NIC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU KWA WATOTO WENYE UONI HAFIFU KITUO CHA ALBINO BUHANGIJA SHINYANGA

Shirika la Bima la taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kujifunzia darasani kwa watoto wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga. Vifaa vilivyotolewa ni darubini kiona mbali(Telescope Monocular),Kikuza Maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bungaja ambaye ndiye msimamizi mkuu wa kituo cha walemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Peter Ajali (katikati),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange ,kulia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez wakijadili jambo kabla ya kukabidhiana vifaa 34 vilivyotolewa na Shirika la Bima la taifa ikiwemo Darubini kiona mbali(Telescope Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)

Mtaalam wa Macho fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter Wilson akiwaelekeza watoto hao namna ya kutumia Darubini Kiona mbali.
Watoto wakifanya majaribio kuhusu matumizi ya darubini kiona mbali.
Mtaalam wa Macho fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter Wilson na Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange wakiwaelekeza watoto hao namna ya kutumia Darubini kiona mbali.
Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima  Makange akimkabidhi  vifaa hivyo na kushikana mkono na msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali
Mwalimu Peter Ajali akiwaonesha wanafunzi wake Darubini Kiona mbali.
Kulia ni Msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akiwaonesha wanafunzi wake moja ya darubini Kiona mbali.
Mtaalam wa Macho Fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter akionesha baadhi ya vifaa hivyo na kueleza matumizi yake
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikagua vifaa hivyo wakati wa makabidhiano. Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Na Kadama Malunde-Shinyanga
*************
Shirika la Bima la Taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kuwasaidia watoto wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino) cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga kutokana na idadi kubwa ya watoto hao kukabiliwa na changamoto ya uoni hafifu.


Vifaa vilivyotolewa  na Shirika la bima la taifa ni pamoja na      Darubini kiona mbali(Telescope Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier).

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo mbele ya mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam, meneja wa Shirika la Bima la Taifa tawi la Shinyanga Halima Makange alisema shirika hilo limeguswa na changamoto ya vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi wenye ulemavu wanaolelewa katika kituo hicho na kuamua kutoa msaada huo.

Alisema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuendeleza elimu kwa watoto hao kwani elimu ni jambo la msingi kwao pamoja na kwamba wanapata hifadhi katika kituo hicho.

“Kilichowaleta hapa watoto hawa ni elimu,tunahitaji kuwaendeleza kielimu ndiyo maana tumeleta vifaa hivi 34,ambavyo vitawasaidia kujifunzia darasani”,alisema Makange.

“Kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la bima la taifa Dar es salaam,nimeleta msaada huu kuungana na jamii kuwasaidia watoto wetu,ingawa vifaa hivi ni vidogo kwa kuviangalia lakini bei yake ni kubwa,tunamshukuru mkurugenzi wetu kwa kuona umuhimu wa kutoa vifaa hivi,naomba vitumike kama vilivyokusudiwa”,aliongeza Makange.


Kwa upande wake mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam alisema vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wenye uoni hafifu waliopo katika kituo hicho cha walemavu.


“Kwanza niushukuru uongozi mzima wa shirika la bima la taifa kwa kunikaribisha kuja kukabidhi vifaa hivi,kwa niaba ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga tunashukukuru sana kwa msaada huu,naomba shirika liendelee kutoa ushirikiano kwa jamii kwani wanatambua nini jamii inahitaji,tutaendelea kushirikiana zaidi”,aliongeza Mukadam.

Naye  Mtaalamu wa Macho Fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Ntoke Sospeter alisema vifaa hivyo vitatumika kuwaendeleza zaidi kimasomo watoto hao ili wafanane na watoto wengine wasiokuwa na tatizo la uoni hafifu.

“Mtoto  asiye ana tatizo la uoni hafifu anaona maandishi mapema zaidi,mwenye uoni hafifu anakuwa na uwezo mdogo wa kufikia maandishi,hivyo tunapompa kifaa tunamsaidia kufikia wenzake wanapofika”,alieleza Dkt Sospeter.

Kwa upande wake msimamizi mkuu wa kituo cha Kulelea watoto wenye Ulemavu wa ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia Peter Ajali alilishukuru Shirika la bima la taifa kwa msaada huo kwani wamelenga kudumisha akili za watoto kimasomo.

Alisema asilimia kubwa ya watoto waliopo katika kituo hicho hawana uwezo wa kuona mbali hivyo vifaa vilivyotolewa vitawasaidia kuweza kuona maandishi kwa ufasaha zaidi.
Na Kadama Malunde-Shinyanga