Tuesday, December 15, 2015

ZIARA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KWENYE KITUO CHA KUZALISHA UMEME KWA NGUVU YA MAJI, MTERA

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametembelea Kituo cha Kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji cha Mtera kwa lengo la kujionea hali halisi ya kituo hicho.

Akielezea hali halisi aliyoiona kituoni hapo, Profesa Muhongo alisema kwa wakati huu kituo hicho cha Mtera hakizalishi umeme wa kiasi chochote huku akitaja sababu kuwa ni upungufu wa maji uliosababishwa na matumizi mabaya ya maji ya Bwawa hilo.

Profesa Muhongo alisema njia bora ya utatuzi wa upungufu wa maji kwenye bwawa hilo la Mtera ambalo hutumiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa ajili ya kuzalisha umeme ni wadau kukaa pamoja na kukubaliana namna ya kutumia maji hayo.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo alitaja utatuzi mwingine kuwa ni kuongeza vyanzo vingine vingi vya kuzalisha umeme mbali na kutegemea maji ili kuruhusu mabwawa hayo kufikia kina kinachohitajika.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia). Kushoto ni Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera, Mhandisi Abdallah Ikwase.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza Mwendesha mitambo ya Mtera, Cosbert Matandu (hayupo pichani). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba na katikati ni Meneja wa Kituo cha Mtera, Mhandisi Abdallah Ikwase. Profesa Muhongo aliagiza chumba cha kuendeshea mitambo ya kituo hicho kifungwe vifaa vya kisasa ili kuboresha utendaji
Moja ya Mtambo wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji wa Mtera wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 40 ukifanyiwa ukarabati. Ukarabati wa Mtambo huo umeanza mwezi huu na unatarajiwa kukamilifika ifikapo mwezi Januari mwakani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza mtaalamu kutoka Bodi ya Maji- Bonde la Rufiji, David Muginya (kulia) akielezea kuhusu mikakati ya matumizi bora ya ili kuhakikisha kila sekta inapata maji.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera, Mhandisi Abdallah Ikwase akimuelezea kuhusu kupungua kwa kina cha maji kwenye bwawa la Mtera.
Muonekano wa Bwawa la Mtera kwa hivi sasa ikionesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kina cha maji.

No comments: