Wednesday, December 16, 2015

WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI LEO

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Ally Mwalimu akiingia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo asubuhi kwa ajili ya kukagua utengenezaji wa mashine ya MRI na CT- Scan.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru leo asubuhi katika hospitali hiyo.
Mtaalamu wa Mionzi kwenye chumba cha mashine ya MRI, Job Joshua (kushoto) na Profesa Mseru (wa pili kulia) wakimpatia maelezo Waziri Ummy Mwalimu (katikati) wakati alipotembelea leo hospitali hiyo kukagua utengenezaji wa mashine hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kwa Mheshimiwa Waziri kuhusu maendeleo ya utengenezaji wa mashine ya MRI leo asubuhi.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na Profesa Mseru kuelekea kwenye chumba cha X-ray cha digitali.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akizungumza leo asubuhi na wagonjwa wanaosubiri vipimo katika hospitali hiyo.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika chumba cha CT-SCAN, huku Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akimpatia maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi wakati ikiwa nzima.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akifafanua jambo baada ya kupewa maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Lawrence Mseru (kulia), Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (katikati) wakimsikiliza mgonjwa aliyefika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu leo asubuhi.

No comments: