Monday, December 14, 2015

Mahafali ya 9 ya Chuo Kikuu Ardhi Yafana, 1874 Wahitimu katika fani mbalimbali

 Mlau (Proctor) wa Chuo Kikuu Ardhi Prof.Joseph Lusuga Kilonde akiongoza andamano la wanataaluma (Academic Procession) wa Chuo Kikuu Ardhi Wakati wa Mahafali ya 9 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Mhe. Cleopa Msuya (kulia) na Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof.Idrissa Mshoro wakiongoza  wahitimu wa Chuo hicho wakati wa Mahafali ya 9, mwaka 2015 jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Mhe. Cleopa Msuya (katikati) na na viongozi wengine wa chuo hicho wakiwaongoza  wahitimu wa  Chuo Kikuu Ardhi na wageni mbalimbali  Kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuwatunuku wahitimu wakati wa Mahafali ya 9 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
 Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Katika fani mbalimbali wakijiandaa kutunukiwa shahada zao wakati wa Mahafari ya 9 yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Mhe. Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamivu ya Chuo Kikuu Ardhi Bw. Mnyone Ibrahim mmoja wa wahitimu 2 wa Digrii ya Uzamivu ya Chuo hicho kufuatia mada ya Utafiti aliyoifanya kuhusu Uendelezaji wa Makazi ya Gharama nafuu kwa ajili ya maisha Bora ya ya Watu wa kipato cha chini.
 Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof.Idrissa Mshoro akizungumza na  wahitimu wa Chuo hicho na hadhara iliyohudhuria  Mahafali ya 9 ya chuo hicho kwa mwaka 2015 jijini Dar es salaam.
Juu na Chini Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi waliohudhuria Mahafali ya 9 ya Chuo hicho katika Ukumbi wa Diamond Jubilee wakifuatilia Matukio mbalimbali. Wahitimu 1874 wametunukiwa Digrii za Uzamivu ,Uzamili,Shahada na  Stashahada za fani mbalimbali katika usimamizi wa Sekta ya Ardhi. Picha na Aron Msigwa-MAELEZO

No comments: