Friday, December 11, 2015

BALOZI ZOKA AWAONGOZA MAAFISA WA UBALOZI KATIKA ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA

Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka akifanya usafi nje ya ofisi yake mjini Ottawa, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi siku ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka, akiwa pamoja na maafisa wa Ubalozi wakitekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli la kusherehekea Sikukuu ya Uhuru na Kazi yaani siku ya tarehe 9 Desemba kwa kufanya kazi na kusafisha mazingira ya Ubalozi.
Mheshimiwa Balozi na afisa wa Ubalozi wakiendelea na usafi.
Mheshimiwa Balozi na afisa wa Ubalozi wakiendelea na usafi.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka, pamoja na maafisa wa Ubalozi wakiendelea na zoezi la usafi nje ya Ubalozi huo.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Jack Mugendi Zoka, akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wa Ubalozi mara baada ya kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli la kusherehekea Sikukuu ya Uhuru na Kazi.

1 comment:

Anonymous said...

Hivi uchaguzi wetu tumepeleka mpaka huko kwa watu?!!!