Na Mwandishi Wetu
WATU
mbalimbali walihudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya
James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market chini ya udhamini wa
Belvedere Vodka, Heineken, Jaguar pamoja na Land Rover.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, mwakilishi wa kampuni ya
QWAY International inayosambaza kinywaji cha Belvedere Vodka,Tanya
Mulamula alisema hafla hiyo inalenga kuwakutanisha wadau na kuifurahia
filamu hiyo, ikiwa siku moja kabla ya uzinduzi wake.
Filamu ya
hiyo ya Spectre iliyoigizwa na Daniel Craig kama James Bond ilizinduliwa
rasmi hapa nchini Ijumaa iliyopita uzinduzi uliofana.
Alisema kuwa
kinywaji hicho kinatambua nafasi ya filamu katika kuwaburudisha wateja
wake na ndio maana imetoa tiketi nyingi za bure kwa wateja wake wengi.
"
Belvedere Vodka, Heineken, Land Rover na Jaguar tumeamua kwa pamoja
kuungana na watu wengine wengi katika kusherehekea uzinduzi wa filamu
hii kwa kuanza na hafla hii ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa
filamu yenyewe" alisema Tanya.
Pia Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya
CMC inayohusika na magari ya Jaguar pamoja na Land Rover, Kim Withnall
alisema kuwa filamu hiyo imehusisha magari ya Jaguar na Land Rovers na
ndio maana hata kwa Tanzania kampuni yake imeshiriki katika kuandaa
hafla hiyo.





Bond Girls posing at the Belvedere Bar
Bond Girls posing at the Heineken DJ Booth.
No comments:
Post a Comment