Friday, October 9, 2015

RAIS NYUSI WA MSUMBIJI AMWANDALIA JK DHIFA MAALUM YA KUMUAGA, JIJI LA MAPUTO LAMTUNUKU UKAZI WA KUDUMU

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi  wa Msumbiji wakigonga glasi ya kutakiana heri wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika ikulu ya nchi hiyo jijini Maputo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa kuamkia leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaaga wananchi wa Msumbiji akisisitiza kuwa uhusiano wa kidugu na kipekee kati ya nchi hizo mbili utaendelea kudumu na kukua
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi wakisimama wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa kuamkia leo.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akimvisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete vazi maalum na kumkabidhi Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo

 Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akijiandaa kumpa  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akishukuru kwa kupewa Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo. Picha na Freddy Maro.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA BUNGE LA MSUMBIJI
Spika wa Bunge la Msumbiji Mh.Veronica Macamo akimkabirisha Rais Kikwete katika bunge hilo,kumtambulisha kwa baadhi ya wabunge na kufanya naye mazungumzo.

 Rais Kikwete akisaini kitabu cha wageni mashuhuri huku Spika wa Bunge hilo Veronica Macamo akishuhudia.

 Rais Kikwete aongea na waandishi wa habari Bungeni Maputo hawapo pichani (picha na Freddy Maro)

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA YA KISEREKALI SIKU MBILI MSUMBIJI

Rais Felipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo wakati alipowasili kuanza ziara ya kiserikali ya siku mbili .

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kwa Rais Felipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji wakipokea heshima  ya Urais wakiwa katika jukwaa maalum(Saluting Dias) na kupigiwa mizinga 21 na kikosi cha jeshi la Msumbiji.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongozwa na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi kukagua  gwaride la heshima lililoandaliwa na vikozi vya Ulinzi vya jeshi la Msumbiji.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji wakipokea maua kutoka kwa watoto na kasha kupia nao picha.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji wakipokea maua kutoka kwa watoto na kasha kupia nao picha.

RAIS KIKWETE NA RAIS NYUSI WAFANYA MAZUNGUMZO MAPUTO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika eneo la mnara wa Mashujaa wa vita vy ukombozi jijini Maputon a kuweka shada la maua(picha na Freddy Maro).

RAIS KIKWETE AWAENZI MASHUJAA WA VITA VYA UKOMBOZI VYA MSUMBIJI

No comments: