Tuesday, October 13, 2015

MWANAHABARI MKONGWE NA MWANDAMIZI AMEINGIA KWENYE KILIMO HAI .


Na Mwandishi wetu
Ni jambo la kawaida kwa mtu yeyote ajira yake inapokaribia kufikia ukomo hufikiria namna atakavyoondesha maisha yake kwa kutafuta shughui itakayo mfanya aweze kujiingizia kipato kwa ajili yake na famiia kwa ujumla .
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Dakta Gideon Shoo (pichani katikati) , mwanahabari mwandamizi na mkongwe ambaye  aliamua kuingia katika kilimo hai cha kisasa  ambacho hakitumii dawa za kemikali kutoka viwandani .
Dakta Shoo kwa sasa kilimo hicho anakifanya nyumbani kwenye shamba katika kata ya Kerege wilayani Bagamoyo mkoa wa pwani .
Akizungumza wakati alipotembelewa shambani na nyumbani kwake  na maofisa kutoka Envirocare , asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na mazingira , hakiza binadamu alisema kilichomhamisha kuingia kwenye shughuli hiyo ni kutokana na kukulia kwenye kilimo .
‘’ Kingine kilichonivuta zaidi ni kwamba nimestaafu . Nikwamba nimestaafu wa maana ya pilikapilika . Kustaafu kwenyewe labda nisababu ya umri . Tangu nimeondoka kwenye ajira rasmi  mwaka 1987 kwenye magazeti ya uhuu na mzalendo sijawahi kuwa tena kuwa kwenye  na ajira rasmi . Nimekuwa nikifanya shughuli zangu mwenyewe . Hata pale watu wanadhani nimekuwa kwenye ajira . Hapana shughuli zangu nazifanya mwenyewe’’ alisema Dakta Shoo .
‘’ Nikasema mimi nadhani sasa nipumzike lakini kupumzika lazima nipate shughui ya kufanya . Shughuli hii nilibuni siku nyingi  nilikuwa nasubiri tu wakati wa kutekeleza . Shughuli hii nilibuni mwaka 1993 -1994 nikiwa na malengo labda mwaka 2000 nitakuwa nimeanza lakini haikuwa hivyo hatimaye nilianza mwaka jana na nikafanikiwa kuhamia huku ‘’ aliongeza
Alisema kabla ya kuhamia hapo tayari alishapanda miti ya matunda ya kudumu . Kupanda miti kwa ajili ya kilimo chenyewe na miti yenyewe ni miarobaini na mirusina .
Mwarobaini ni mti ambao unachangia kuendeleza kilimo cha kisasa ambacho hakitumii dawa za viwandani :
‘’Mwarobaini ni dawa na umekuwa ukitumika kwa kilimo nchini India tangu kabla ya kuzaliwa kwa  yesu kristo na hakuna haja ya kufanya utafiti kwasababu wahindi tayari walishaufanya ‘’ alisema Dakta Gideon Shoo mkulim  katika kata ya Kerege wilayani Bagamoyo .
Amesema wahindi wamefanya utafiti kwa miaka mingi sana kiasi kwamba unapozungumzia kilimo cha kisasa cha kutotumia dawa za kuuwa wadudu za viwandani hakuna haja ya kufanya utafiti mwingine kwani wahindi walishamaliza .
 ‘’ Mwarobaini mbegu yake inatoa mafuta ambayo yanauwezo wa kuuwa wadudu na magonjwa aina 600  . Kwa kiasi kikubwa uchanganyaji wake ni rahisi tu . Mafuta unachanganya na sabuni ya unga kidogo na  kupulizia kwenye mmea bila matatizo yeyote . Kwahiyo mwarobaini ni mti naupenda na niliupanda kwa miaka mingi nikiwa na malengo hayo  ‘’ alisema .
Mwarobaini unachofanya ni kufubaza wadudu wasiwe na uwezo tena wa kufanya madhara na pia wakati huo huo majani yake yanatumika kuuwa vijidudu vilivyoko kwenye udongo . Kwa hiyo nimehamasika na nakifanya kilimo hiki nikiwa na imani kwamba nitapata mafanikio na watu wengine wanaweza kuiga .
Kinachomsaidia pia mkulima huyo kutotumia mbolea ya kemikali ni kwamba mimea iliyoko kwenye shamba lake majani yake yanapeekwa kwenye chemba ili yaweze kuoza na kupelekwa kwenye biogas ambapo pia anapata mbolea .
‘’  Hatutegemei ufugaji wakati unapopata gesi kwa upande mwingine unapata mbolea  kwasababu yale maji yanayotoka kwenye mtambo wa gesi ni mbolea na ndio natumia kumwagilia mimea na jinsi unavyoona mimea imestawi ni mbolea iiyotoka kwenye mtambo wa gesi ‘’
Amesema wakati anaposafisha mtambo kuna mbolea ngumu inatoka ambayo ni chakula cha samaki ambacho anatarajia kuwalisha wakati akianza kuwafuga .
‘’ Mimi nina mabwaya ya samaki ambayo sijaweka maji nasubiri kuchimba visima na kujaza maji nifuge samaki . Kwahiyo unaona kuna mzunguko hapa eneo moja linategemea eneo linguine ‘’
Amesema changamoto inayowakabili wakulima ni kutokuwa na maabara ya kupima udongo ambayo inatoa majibu ya haraka .
‘’ Unaweza mbolea ukamimina tu kumbe unaharibu . Udongo unakuwa labda potassium imezidi au imepungua calcium au imepungua phosphorous nakuendelea .
Sasa hivi . Napeleka Nairobi . Najua watu watasema mbona kuna SUA au Mlingano . Kwasababu ukipeleka udongo jumatatu siku ya alhamisi unapata majibu . Wako kwenye biashara na sisi hapa Tanzania sijui kama tunazo maabara ambazo zinafanya shughuli hiyo kwa namna hiyo . Bado hatujafika huko kuna changamoto .
Amesema katika kuondokana na changamoto hiyo ameagiza mashine ya kupima udongo kutoka India na kazi ya kupima ataifanya shambani kwake ambapo hatakuwa na kazi tena ya kupeleka udongo mahali popote kupimwa .
‘’ Changamoto hiyo nadhani serikali lazima iibebe . Haiwezi kukwepa jukumu lake la kuendeleza kilimo kwa kuangalia vitu vya msingi ikiwemo pia upatikanaji wa maji  ambavyo vitamsaidia  mtu anayetaka kulima  katika eneo dogo aweze kuzalisha zaidi badala ya serikali  kukimbilia kwenye matrekta .’’
Changamoto ya kuwepo kwa maabara za kupima udongo ambazo zinaleta majibu ya haraka pia imeungwa mkono na Mkurugenzi mtendaji wa Envirocare bibi Loyce Lema ambaye pia ameshauri serikali isaidie katika upatikanaji wa maofisa ugani watakaosaidia wakulima kutambua udongo unaofaa kwa ajili ya kupanda mazao fulani .
‘’ Ni vuri mkulima akajua udongo wake uko katika kiwango gani na unavirutubisho gani ili kama vimepungua aweze kuongeza kilichopungua katika udongo .  Mara nyingi sana sisi watanzania tunalima tu kwasababu tu umeona ni udongo . Unaona unaweza kuzalisha kwa hiyo mwisho wa siku hautavuna chechote .
Kwa hiyo tungeambiwa udongo wetu una matatizo gani na tukaweza kuuboresha tungeweza kuvuna sana. 
Tunataka kuiomba serikali itusaidie kutupatia maofisa ugani watakaosaidia kuwaelimisha wakulima kujua udongo umepungua kiasi gani ‘’ aliomba Bi. Loyce .
Kuhusu kilimo hai amesema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kuna mambo mengi yametokea katika mazingira ikiwemo wadudu kuongezeka kwa hiyo ili wakuma waweze kuvuna lazima watumie viwatilifu .
‘’ Wako wachache ambao wanalima kidogo wao wanaweza kulima bila kutumia viwatilifu .  Sasa hivi sisi envirocare tunahamasisha wakulima kulima hasa majumbani kwao . Wanaweza kulima kwa ajili ya familia bila kutumia viwatilifu kama tulivyoona nyumbani hapa kwa Dakta Shoo ambaye ameweza kulima kwa ajili ya familia yake na hata majirani . Ametuonyesha kwamba ukiwa na ndoo chache unaweza ukalima kwa ajili ya familia’’ aliongeza .
Kwa upande wake bibi Euphrasia Shayo , Meneja wa mradi wa wiki ya kijani kutoka envirocare amesema wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kula vyakua vinavyotokana na kilimo hai .
‘’ Tumeona pia magonjwa mengi watu wanapata kutokana na ulaji wa vyakula vinavyotokana na matumizi ya  kemikali zenye sumu kutoka viwandani . Kwahiyo tunahamasisha jamii iweze kulima bila kutumia dawa au mbolea ya viwandani ‘’ alisema bi. Euphrasia .
Kitendo cha envirocare kumtembelea mkulima huyo ni sehemu ya  wiki ya kijani ambayo inafanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi septemba hadi oktoba kwa ajili ya kuhamasisha kilimo hai ambacho hakitumii sumu ya kemikali kutoka viwandani .

Wiki hiyo imeandaliwa na  shirika lisilo la kiserikali la Swedish Society for Nature  Conservation ambapo   familia zinahamasishwa kulima vishamba vidogo katika maeneo yao kwa kupanda mbogo ambazo ni safi na salama na pia kusaidia kupunguza gharama za kwenda kununua mboga . 

No comments: